Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” mwishoni mwa mwezi huu itafanya ziara ndefu ya maonyesho katika mikoa ya nyanda za juu kusini.
Twanga Pepeta itaanzia ziara yake NJOMBE siku ya Jumatano tarehe 26-03-2014 katika ukumbi wa Turbo. Siku inayofuata tarehe 27-03-2014 siku ya Alhamisi kwa mara ya kwanza kabisa watakuwa Wilaya mpya ya MBABABAY katika ukumbi wa BAY LIVE SOCIAL HALL.
Ziara ya Twanga Pepeta siku ya Ijumaa tarehe 28-03-2014 itahamia Songea mjini katika ukumbi wa Serengeti. Siku ya Jumamosi tarehe 29-03-2014 itakuwa ni zamu ya Jiji la Mbeya katika ukumbi wa City Pub.
Maandalizi ya ziara yanaendelea vizuri na Twanga Pepeta imejitayarisha vilivyo kukonga nyoyo za mashabiki watakaojitokeza katika maonyesho yake.
Twanga Pepeta itatumia ziara hii kuitangaza albamu yake mpya ya Nyumbani ni Nyumbani pamoja na kupiga nyimbo zilizopo kwenye albamu zake 12.
0 comments:
Post a Comment