Wednesday, March 12, 2014


AMIRKAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ilifanya kikao chake cha kwanza chini ya uenyekiti wa Juma Pinto juzi Jumatatu Machi 10, 2010 jijini Dar es Salaam na kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali.       
1; MAFUNZO
Kikao kilikubaliana kuelekeza nguvu katika mafunzo kwa wanachama wake na kwa kuanzia kamati iliagiza sekreterieti ya TASWA ihakikishe inasimamia hilo kwa nguvu zote ili kuboresha uwezo wa namna ya kuripoti michezo mbalimbali hasa kwa waandishi chipukizi.
Katika hilo bajeti maalum itaandaliwa kwa ajili ya kuona namna ya kushirikiana na wadau mbalimbali watakaosaidia mafunzo hayo ikiwemo Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS).
2;Media Day
Kama inavyojulikana kwamba kila mwaka TASWA inaandaa bonanza maalum likihusisha waandishi na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Mwaka huu Kamati ya Utendaji imepanga lifanyike Mei 10 jijini Dar es Salaam katika eneo ambalo lina fukwe nzuri. Hivyo tayari watu maalum wameshateuliwa kufanya utaratibu wa mahali litakapofanyika.
Pia mazungumzo na wadhamini mbalimbali kuhusu bonanza hilo litakaloenda sambamba na sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yameanza na yana muelekeo mzuri, ambapo litashirikisha waandishi wa habari na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari 2,000.
3;Tuzo za Wanamichezo Bora
TASWA imeunda kamati maalum ya kusimamia tuzo hiyo na kuifanya iwe bora pengine kuliko za miaka iliyopita. Majina ya kamati hiyo tutayatangaza baada ya wote kuwa wameshapatiwa barua zao za uteuzi na kuzijibu. Tarehe ya tuzo ni baada ya kamati kukutana na ndiyo itakayopendekeza kulingana na majukumu iliyopewa.
4; Marekebisho ya Katiba
Pia kikao kilikubaliana kuelekeza nguvu katika marekebisho ya katiba ya chama. Katika kufanikisha hilo imeundwa kamati maalum kwa ajili ya jambo hilo. Majina ya kamati hiyo pia yatatangazwa baada ya wote kuwa wameshapewa barua zao na kujibu kwa maandishi.
5;SACCO’S
 Kwa kuwa suala hili lilishapitishwa kwenye Mkutano Mkuu wa chama Desemba 2012, kikao kilikubaliana lifanyiwe kazi na utekelezaji uanze sasa.
Utaratibu unaandaliwa kuhusiana na jambo hilo baada ya kupata mwongozo kutoka vyama vya ushirika, kisha wanachama wa TASWA watajulishwa na wale watakaopenda kujiunga watapewa maelekezo kwani hilo ni jambo la hiyari kwa yule atakayependa.
6: Uhai wa chama
Suala la uhai wa chama lilichukua nafasi kubwa, hivyo utaratibu maalum utawekwa kuhamasisha waandishi wa habari za michezo hasa wale wa mikoani kujiunga na chama.
Ili kuweka mkazo jambo hilo, baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA na baadhi ya wanachama watapewa fursa kwa ufadhili wa chama kusafiri maeneo mbalimbali mikoani kuhamasisha waandishi wa huko kujiunga na chama.
Ahsante.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
12/03/2014

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video