- WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUPINDUKA
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WAKIWA NA POMBE HARAMU YA POMBE.
- MTU ASIYEFAHAMIKA ATELEKEZA SILAHA HUKO KATIKA KIJIJI CHA UTAMBALILA.
WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE WATATU KUJERUHIWA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUPINDUKA.
MNAMO TAREHE 07.03.2014 MAJIRA YA SAA 10:00HRS ASAUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIWIRA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.985 BPC AINA YA TOYOTA DYANA LILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA WILLY AGENCY MANGUNGURU UMRI KATI YA MIAKA 35-38, MKAZI WA KATUMBA–TUKUYU LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MARY ANYELWISYE (51) MKAZI WA KIJIJI CHA KIKOTA NA KUFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MISHENI IGOGWE. AIDHA MARA BAADA YA TUKIO HILO GARI LILIPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI KWA ABIRIA WANNE WALIOKUWA NDANI YA GARI HILO KATI YAO REBY MWAIKENDA (40) MKAZI WA RUNGWE ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA MISHENI IGOGWE. MAJERUHI WALIOKUWEMO KATIKA GARI HILO NI PAMOJA NA 1. LUGANO JANKEN (24) MKAZI WA KIKOTA 2. REO MWASEBA (74) MKAZI WA KYELA NA 3. ALEX PHILIPO (25) MKAZI WA KATUMBA AMBAO WOTE WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI IGOGWE. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WAKIWA NA POMBE HARAMU YA POMBE.
WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. LATARO KASIUPA (42) 2. ULIMBOKA MICHAEL (35) 3. SOPHIA ATUPELE (25) NA 4. VENUS OMARY (25) WOTE WAKAZI WA IGURUSI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [05]. WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 06.03.2014 MAJIRA YA SAA 17:00HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
MTU ASIYEFAHAMIKA ATELEKEZA SILAHA HUKO KATIKA KIJIJI CHA UTAMBALILA.
MNAMO TAREHE 07.03.2014 MAJIRA YA SAA 10:45HRS ASUBUHI JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LIKIWA KATIKA MSAKO HUKO KATIKA KIJIJI CHA UTAMBALILA, KATA YA NAMBINZO, TARAFA YA ITAKA, WILAYA YA MBOZI LILIFANIKIWA KUKAMATA SILAHA MOJA BUNDUKI AINA YA GOBOLE INAYOTUMIA RISASI ZA GOROLI IKIWA IMETELEKEZWA KWENYE PAGALA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI JUU YA MTU/WATU WANAOMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA ILI WAKAMATWE NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI, VINGINEVYO WASALIMISHE WENYEWE SILAHA HIZO.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment