Friday, March 7, 2014

DSC00207
“PRESS RELEASE” TAREHE 07.03.2014.
  • BASI LA KAMPUNI YA SAIBABA LAPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI WILAYANI RUNGWE.
  • MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGOGWA NA GARI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI.
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MKAZI WA MTAA WA ILOLO AKIWA NA MICHE YA BHANGI PAMOJA NA POMBE HARAMU YA MOSHI NA MITAMBO YA KUTENGENEZEA POMBE HIYO.
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA DAWA ZA KULEVYA AINA YA BHANGI.
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MKAZI WA MTAA WA ILOLO AKIWA NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
BASI LA KAMPUNI YA SAIBABA LAPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI WILAYANI RUNGWE.
BASI LA KAMPUNI YA SAIBABA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.973 AVM AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE  LIKITOKEA DSM KUELEKEA KYELA LILIPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA ABIRIA MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE BAADA YA KULALIWA NA BASI HILO. AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 07.03.2014 MAJIRA YA SAA 00.10HRS USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUKUYU KATIKA KIJIJI CHA MWAMBEGELE, KATA YA KYIMO, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE.  AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU NANE [08]WALIJERUHIWA KATI  YAO WANAUME WAWILI [02] NA WANAWAKE SITA [06] WOTE WAMELAZWA HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA – TUKUYU. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA NA KONDAKTA WALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.
MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGOGWA NA GARI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI.
MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA  KIUME, UMRI KATI YA  MIAKA 12-14  ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGOGWA NA  GARI AMBALO HALIKUWEZA KUFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI WALA DEREVA WAKE. AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 06.03.2014 MAJIRA YA SAA 09:00HRS ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MLIMA MPEPO, KATA YA IGOMA, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI KATIKA BARABARA YA ISYONJE/MAKETE. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA HASA WATEMBEA KWA MIGUU KUWA MAKINI WANAPOTUMIA BARABARA KWA KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA NA KUVUKA KATIKA SEHEMU ZENYE VIVUKO [ZEBRA CROSSING] ILI KUEPUKA AJALI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MKAZI WA MTAA WA ILOLO AKIWA NA MICHE YA BHANGI PAMOJA NA POMBE HARAMU YA MOSHI NA MITAMBO YA KUTENGENEZEA POMBE HIYO.
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ATHANAS   MASINJARA (64) MKAZI WA ILOLO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA AMEPANDA BHANGI MICHE 12 YENYE UREFU WA FUTI NNE KATIKA SHAMBA LAKE LA MAHINDI.MTUHUMIWA BAADA YA KUKAMATWA NA MICHE HIYO, UPEKUZI ULIFANYIKA KATIKA NYUMBA YAKE NA KUFANIKIWA KUKUTA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA MBILI [02] PAMOJA NA MITAMBO MIWILI YA KUTENGENEZEA POMBE HIYO HARAMU. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 06.03.2014 MAJIRA YA SAA 11:45HRS ASUBUHI HUKO KATIKA MTAA WA ILOLO, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI. MTUHUMIWA NI MTENGENEZAJI/MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE/BHANGI, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI PAMOJA NA DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
JESHI LA PSI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA BHANGI.
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NEEMA NICEMBO (32) MKAZI WA NZOVWE AKIWA NA BHANGI KETE 26 SAWA NA UZITO WA GRAM 130. MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 06.03.2014 MAJIRA YA SAA 17:30HRS JIONI HUKO KATIKA MTAA WA NZOVWE, KATA YA NZOVWE, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KWA KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MKAZI WA MTAA WA ILOLO AKIWA NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MWANAMKE MMOJA MKAZI WA MTAA WA ILOLO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ZENA SAID (30) AKIWA NA MTAMBO MMOJA WA KUTENGENEZEA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 06.03.2014 MAJIRA YA SAA 11:45HRS ASUBUHI HUKO KATIKA MTAA WA ILOLO, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KWA KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI IKIWA NI PAMOJA NA WANAOMILIKI MITAMBO YA KUTENGENEZEA POMBE HIYO ILI WAKAMATWE NA HATUA KALI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video