- MPANDA BAISKELI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBOZI.
- MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI RUNGWE.
- JI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA BHANGI
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
- MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SITA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
MPANDA BAISKELI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBOZI.
GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.953 BJL AINA YA NISSAN MALI YA KAMPUNI YA USAFIRISHAJI YA SUMMRY LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA FURAHA JONAS (32) MKAZI WA SUMBAWANGA, LILIMGONGA MPANDA BAISKELI AITWAYE SIMON PHILIPO @ SIAME (25) MKAZI WA KIJIJI CHA CHIMBUYA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 05.03.2014 MAJIRA YA SAA 17:00HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHIMBUYA, KATA YA MPEMBA, TARAFA YA CHIMBUYA, WILAYA YA MBOZI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO CHA POLISI VWAWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA HASA WATEMBEA KWA MIGUU KUWA MAKINI WANAPOTUMIA BARABARA KWA KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA NA KUVUKA KATIKA SEHEMU ZENYE VIVUKO [ZEBRA CROSSING] ILI KUEPUKA AJALI.
MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI RUNGWE
MWENDESHA PIKIPIKI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FURAHA KASALILE (29) MKAZI WA KIJIJI CHA KIKITA ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.969 AQY AINA YA SLG ALIGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.165 CLK AINA YA TOYOTA NOAH ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 05.03.2014 MAJIRA YA SAA 14:00HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIKITA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE. CHANZO CHA AJALI NI MWENDESHA PIKIPIKI KUJARIBU KUYAPITA MAGARI YALIYOKUWA MBELE YAKE BILA KUCHUKUA TAHADHARI. DEREVA WA GARI ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA BHANGI.
WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. MESHACK KILUMBILE (23) NA 2. HAMZA ABDALAH (30) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IHANGA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI UZITO WA GRAM 500. WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 05.03.2014 MAJIRA YA SAA 04:05HRS ALFAJIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MKANYAGENI, KATA YA RUJEWA, TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA MBARALI. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
WATU WATANO WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. RAHABU SHADRACK (31) MKAZI WA KIJIJI CHA KALASHA 2. SIKUJUA JACKSON (40) MKAZI WA KIJIJI CHA IBILILO 3. ANYASIME WILLISON (36) MKAZI WA KIJIJI CHA KIKOTA 4. LUCAS HEZRON (25) MKAZI WA KIJIJI CHA KIWIRA 5. SIMON HEBRON (25) MKAZI WA KIJIJI CHA KIKOTA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA KUMI [10]. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO 05.03.2014 MAJIRA YA SAA 13:30HRS MCHANA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA LUKWEGO, KIJIJI CHA KARASHA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE WILAYA YA RUNGWE. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SALVATORY MWANKENJA (34) MKAZI WA KIJIJI CHA KIKOTA AKIWA NA BHANGI KETE NNE [04] SAWA NA UZITO WA GRAM 20. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIENDESHWA NA JESHI LA POLISI MNAMO TAREHE 05.03.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIKOTA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI.
JESHI LA POLISI MKOA LINAWASHIKILI WAFANYABIASHARA WAWILI 1. PHILIPO MWAISANILA (27) MKAZI WA MAKUNGULU NA 2. KELVIN JAPHET (28) MKAZI WA MWANJELWA WAKIWA NA MADUMU 40 YA DAWA YA KUSAFISHIA MADINI AINA YA SOLID YAKIWA YAMEPAKIWA KWENYE GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.948 AEL AINA YA CANTER MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI. WAFANYABIASHARA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 05.03.2014 MAJIRA YA SAA 21:00HRS USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA KAWETERE, KATA YA MWANSEKWA, TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA SHUGHULI HARAMU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WATAFUTE KAZI HALALI ZA KUFANYA ILI WAJIPATIE KIPATO NA KUENDESHA MAISHA YAO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SITA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
KATIKA MSAKO ULIOENDESHWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA MNAMO TAREHE 05.03.2014 MAJIRA YA SAA 19:00HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KATUMBA, KATA YA IBICHI, TARAFA YA UKUKWE WILAYA YA RUNGWE, WATUHUMIWA SABA WALIKAMATWA AMBAO NI 1. GEOFREY MWAKIPESILE (41) 2. BONIFACE MWAKAMBOJA (29) MKAZI WA KIJIJI CHA LUSANJE 3. ATHUMANI MWANKOTWA (31) 4. MOSES ARON (21) 5. FURAHA MWANDEBI (40) 6. MUSA GEORGE (28) 7. BONIFACE JOSEPH (19) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA KATUMBA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [05]. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI NA WAUZAJI WA POMBE HIYO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment