TOTTENHAM ikiwa katika moto kwasasa chini ya kocha wake Tim Sherwood imeilaza mabao 3-2 Southampton katika mchezo wa ligi kuu soka nchini England.
Bao la dakika 90 la Gylfi Sigurdsson limewafanya Tottenham wapumue na kuibuka na ushindi muhimu zaidi leo.
Mabao mengine ya Spurs yamefungwa na Christian Eriksen katika dakika 31 na 46.
Mabao ya Southampton yalifungwa katika dakika ya 19 kupitia kwa Jay Rodriguez na dakika ya 28 kupitia kwa Adam Lallana
Kikosi cha Spurs leo hii: Lloris 6; Naughton 4, Kaboul 5, Vertonghen 5.5, Rose 6; Dembele 5 (Sigurdsson 46, 7), Bentaleb 6; Lennon 6 (Townsend 71) Eriksen 8, Chadli 5; Soldado 6.5
Kikosi cha Southampton: Boruc 6; Clyne 5.5 (Chambers 46, 5.5), Lovren 5, Fonte 5.5, Shaw 6; Davis 6, Cork 6, Lallana 7.5; Ward-Prowse 6, Rodriguez 6.5 (Ramirez 63, 6); Lambert 7 (Gallagher 89)
Msumari wa mwisho: Gylfi Sigurdsson alifunga bao la ushindi kwa Tottenham dhidi ya Southampton
Mshindi: Akitokea benchi, Sigurdsson alishangilia kwa furaha baada ya kuifungia bao la ushindi Spurs
Msawazishaji: Christian Eriksen (kushoto) na Roberto Soldado wakipongezana baada ya kufunga bao la pili leo hii
Mtu chali!: Christian Eriksen (kulia) akitia kambani bao la pili la kusawazisha la Tottenham
Mfungaji wa bao la kwanza leo: Jay Rodriguez (katikati) akimfunga kipa wa Spurs Hugo Lloris kufunga na kuwapa Southampton bao la kuongoza
Nzuri sana kaka! Rodriguez (jezi namba 9) anapongezwa na Lallana baada ya kufunga bao
0 comments:
Post a Comment