
“Kwa niaba ya Wabunge wote, napenda kutoa salamu za rambirambi kwako, familia ya Marehemu na Wananchi wote wa Mkoa wa Mara kufuatia msiba huu mkubwa.
Marehem John Gabriel Tupa atakumbukwa kama kiongozi shupavu, mwadilifu na mchapa kazi hodari katika nyadhifa mbalimbali alizowahi kuzitumikia wakati wote wa uhai wake.
Tumwombe Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.” Inamaliza taarifa ya Spika.
Marehemu Tupa alizaliwa tarehe 01 Januari, 1950 na katika enzi za uhai wake amewahi kuongoza Wilaya za Chunya, Mwanga, Bukoba, Muleba na Dodoma kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mwaka 2011. Ameacha Mke na watoto watano.
Imetolewa na;
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa
0 comments:
Post a Comment