Na Omary sadick Kuhanzibwa.
Wakati uso wasaa ya
dunia unaenda kasi sana, huku nao wana sayansi wakiumiza kichwa kuhusu ndege ya
Malaysia iliyopotea, nayo Brazili ikiwa na maombolezo ya nahodha wake aliyewaisaidia kutwaa kombe la dunia pale Sweeden 1950 , wakati huo huo sherehe ya mzee Arsene
wenger kutimiza mechi 1000 zikishereheshwa kwa kipgo kibaya cha goli 6-0 kutoka
kwa Chalsea, bado uso wa saa wa dunia ukasema kwa nini Manchester United wakiwa
mabingwa wa EPL wasistahili kukutana na bingwa mwingine wa Bundesliga ,Bayern Munchen. The Bavarians.
Luis Figo,
nguli wa zamanI wa Barcelona , Real Madrid na Ureno huenda ameingia kwenye
orodha ya watu ambao pengine wanachukiwa na mashabiki wa Man u, hiii ni
kutokana na Droo ya robo fainali ambayo Figo alikuwa balozi wake .
Katika droo hiyo, klabu ya Manchester United imepangwa kucheza
na bingwa mtetezi wa kombe hilo Buyern
Munich, huku wenzao Chelsea wakipangwa dhidi ya Paris saint Germain ya nchini
ufarasa.
Lakini tukio lililoshika
hisia za watu wengi, na kuchafua mapumziko ya mwisho ya wiki kwa mashabiki ni
hili la Mancheste united.
Mashabiki
wengi kama sio wote, wakurugenzi, hata jopo la ufundi la Man United, na
hata wachambuzi na waandishi mbali mbali wa habari za michezo wasingetamani Mashetani wekundu kwa hali waliyo nayo kukutana na
Bayern ya Pep Guardiola.
Kweli Man United ataweza kuwatafuna wanaume hawa?
Si kwamba timu hizi ndio zinakutana kwa mara ya
kwanza, la hasha..! kwa mujibu wa vyanzo vya habari, timu
hizi zimekutana takribani mara 9.
Manchester United imefanikiwa kushinda mara 2,
kutoka sare mara 4 na kufungwa mara 3, huku tukio linalokumbukwa na watu wengi na
linalowapa matumaini si mashabiki hata wachezaji wa sasa wa Man United na
viongozi wao, ni hili la mwaka 1999 katika fainali hizo ambapo Manchester ikiwa
chini ya koch Sir Alex Ferguson ilishinda na kutwaa taji hilo.
Mwari huyo!: Kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya likiwa limewekwa Nyon, Switzerland wakati wa droo
Mara ya mwisho kukutana
ni mwaka 2010 katika hutua kama hii ambapo Manchester United waliondoshwa kwa
goli la ugenini, lakini kutokana na hali
ya sasa ya Manchester united ambayo ni mbaya, wapo nafasi ya saba kulinganisha
na hawa ambao wameshafikia asiliia 99 kutwaa ubingwa nchini kwao na hivyo
kuhamishia mawazo yote katika kutetea ubingwa huo wa ligi ya mabingwa barani
ulaya, kumesababisha mchezo huo kuwa gumzo katika medani ya soka.
Pamoja na hayo yote
mpira ni dakika 90, mpira ni mchezo wa maajabu makubwa. Kuna wakati timu ambayo
haipewi nafasi inaweza kufanya maajabu.
Kuna baadhi ya matukio
ya kihistoria katika medani hii ya soka yaliyopata kutokea mfano wake ni haya
yafuatayo;
Tukianza hapa barani
Afrika maeneo ya afrika mashariki nchini Tanzania tunaikuta klabu moja ya simba
ya jijin dare s salaam.
Mnamo mwaka 2003,
katika michuano ya klabu bingwa afrika, Simba ilipangwa kucheza dhidi ya bingwa
mtetezi, klabu ya Zamaleck ya nchini Misiri.
Kutokana na ugumu wa mchezo
wenyewe watu wengi hata Wamisri nao waliamini watasonga mbele hii ni kwasababu timu
ya Simba haikupewa nafasi kubwa kutokana na kikosi bora cha wapinzani wao.
Wakati huo Simba
ilikuwa na wakali kama akina Suleiman Matola, Emmanuel Gabrile Mwakyusa, beki
mahiri Boniphace Pawasa, Victor Costa Nyumba,
Juma kaseja, na wengene wengi chini ya kocha Mkenya James Agrey Siang’a.
Wamevurugwa: Wayne Rooney na Manchester United watautafuna mfupa wa Bayern Munich?
Si kwamba Simba walikuwa
na kikosi kibovu, kikosi chao kilikuwa imara lakini si kama kile cha wapInzani
wao, mwisho wa siku Simba ilisonga mbele na kufanikiwa kuingia hatua ya
makundi.
Hata huko barani ulaya,
nani aliyeamini kuwa Chelsea wanaweza kutwaa taji hilo? mashabiki wengi wa Chelsea
walikata tamaa toka hatua ya nusu fainali waliposikia wamepangiwa Barcelona, lakini mwisho wa siku walitinga fainali
wakacheza dhidi ya kikosi hiki kinachoenda kucheza dhidi ya manichester united
hatua ya robo fainali.
Goli zuri la Didier Drogba liliitoa matumaini ya kutwaa taji hilo
kwa kuifunga Bayern kwa njia ya penati kutokana na timu hizo kumaliza dakika 120
zikiwa zimefungana goli 1 kwa 1.
Mpira si uchawi wala si
maneno, bali ni mbinu unazozitumia dhidi
ya wapinzani wako, hata uwe na kikosi bora zaidi lakini kama ukikosa mbinu ya kukitumia kikosi hicho,
sitashangaaa kutokea kama yale yaliyotokea kwa simba dhidi ya zamaleck, au
Chelsea na Bayern Munich 2012.
Wachambuzi wengi wa soka wanaikosoa MAN U .kwamba imeshuka morali na kiongozi
wawapo uwanjan , na wamekuwa wakikosoa mbinu na mfumo usioeleweka wa kocha
Moyes , kitu ambacho kitampa ugumu mwalimu mwenye falsafa ya `tikitaka` Pep Guardiola
kujua ni mfumo upi unastahili kuwakabili
man U..
Maajabu ya Man U
kupindua matokea ambayo yamekuwa kama miujiza kwa wengi ambao waliona ni kama
ngamia kupenya kwenye tundu la sindano , baada ya mchezo wa kwanza kulala 2 -0
na Olympiakos kule Ugiriki na kufuatiwa na kiwango cha hali ya juu cha
wachezaji kama Giggs,Valencia, Rooney , Ferdinand na Robin Van Persie ambaye kwa bahati mbaya
hatakuwepo kwenye michezo yote miwili ya mikondo ya robo fainali.
Inawezekana kwamba Man
U inayopewa nafasi finyu inaweza
kuiondoa Bayern ambayo inatazamiwa kuwepo pale Porto katika fainal na kunyakua
tena kombe hilo .
2 comments:
Sio kweli kwamba Chelsea walikata tamaa baada ya kupangiwa kukutana na Barcelona.Je wajua ni timu katika EPL inayo itesa Barcelona,ni Chelsea wazee wa darajani.Kwahi hiyo Man U wanaouwezo wa kuwapiga Baryen Munich.
Mpira wa miguu ni mchezo wa ajabu yule umzaniae kuwa ndie mara nyingine huwa siyo.Ni mtazamo wangu tu huo,siku njema.
Asante kwa maoni yako. Tunashukuru sana na karibu sana
Post a Comment