Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
0712461976/0764302956
MASHINDANO ya madarasa (Inter-Class Competitions) chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) yanatarajia kuanza siku chache zijazo kwa lengo la kupata kikosi kitakachoiwakilsha shule hiyo katika mashindano ya vyuo na shule za Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM).
Kiongozi wa michezo wa SJMC, George Owino amesema maandalizi yameanza, na mapema wiki ijayo watakuwa na kikao na wawakilishi wa madarasa yote matatu.
“Jumanne ya wiki ijayo tunatarajia kukutana na wawakilishi wa madarasa. Mwaka wa kwanza watawakilishwa na Haruna Ramadhan Ngoda, mwaka wa pili atakuwepo Issa Rashid na mwaka wa tatu Peter Mabere. Lengo ni kujadili jinsi ya kuyafanya mashindo yawe na mvuto”. Alisema Owino.
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mashindano ya SJMC nA Muakilishi wa mwaka wa tatu katika kikao, Peter Mabere `Balotelli` amesema uteja kwa SJMC katika mashindano ya Chuo (inter-college competition) sasa basi, mwaka huu watajenga kikosi cha hatari.
“Mkuu wa Chuo alituahidi vifaa mwezi huu wa tatu, hivyo kuanzia wiki ijayo tutamkumbusha. Matumaini ya kupata vifaa ni makubwa sana. Ukweli kwasasa jezi hazipo na mpira uko mmoja tu”
Naye mjumbe wa kamati ya maandalizi, Peter Mabere maarufu kwa jina la Mario Balotelli amesema lengo lao mwaka huu ni kupata timu ya ushindani katika mashindano makubwa ya chuo kikuu cha Dar es salaam ili kuleta upinzani mkubwa tofauti na miaka ya nyuma.
Mjumbe wa kamati ya maandalizi na muakilishi wa mwaka wa pili katika kikao cha kamati ya maandaliz ya mashindano SJMC ambaye pia ni mchezaji nyota wa kikosi cha mwaka wa pili, mabingwa watetezi wa mashindano hayo , Issa Rashid amesema mwaka huu watatoa vipigo vikubwa kwa wapinzani wao.
Jembe la kazi Frank Joseph (wa kwanza kushoto), Peter Mabere (wa pili kushoto), Issa Rashid (wa tatu kushoto) na Mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi SJMC -DARUSO, Michael Christopher (kwa kwanza kutoka kulia).
Jembe la kazi Frank Joseph (wa kwanza kushoto), Peter Mabere (wa pili kushoto), Issa Rashid (wa tatu kushoto) na Mwenyekiti wa serikali ya wanafunzi SJMC -DARUSO, Michael Christopher (kwa kwanza kutoka kulia).
“Unajua sisi mara nyingi
tumekuwa washiriki katika mashindano haya kutokana na upinzani wa baadhi ya
vyuo kama CASS, COET n.k. Lakini mwaka huu tunataka kuanza mashindano ya ndani
ya shule yetu ili kupata wanandinga bora kutoka mwaka wa kwanza mpaka wa tatu na
kuunda kikosi cha kazi. Ubingwa ni wetu mwaka huu”. Alisema.
`Balotelli` ambaye ni
mchezaji hatari kwa mwaka wa tatu.
Pia aliwaomba wachezaji wa darasa lake kujiandaa
kusaka namba katika kikosi cha mwaka huu kwani ushindani ni mkubwa.
Issa Rashid, mchezaji na
muawalikishi wa mwaka wa pili alisema kuwa kwa vijana wake ambao ni mabingwa
watetezi wa mashandano ya mwaka jana chuoni hapo, wapo tayari kuonesha cheche
zao kama kawaida.
“Sisi ni wazee wa vipigo,
lazima wajue hilo. Kikosi chetu kipo imara, wachezaji wapo katika morali kubwa
sana. Mashabiki wakae mkao wa kupata soka bora kutoka kwa mwaka wa pili.”.
Alisema Issa.
0 comments:
Post a Comment