Monday, March 10, 2014

SIKIA kwanza. Simba imemaliza kazi kwenye ardhi ya Mbeya, haitaonekana tena kwenye Uwanja wa Sokoine mwaka huu katika mechi za Ligi Kuu Bara.
Ilipanda ndege ya kwanza ikaenda Mbeya kuifuata Mbeya City ikaambulia pointi moja ikapanda dege lingine kurudi Dar es Salaam. Wiki iliyopita ikainuka tena kwa ndege kuifuata Prisons ikaambulia pointi moja jana Jumapili na leo Jumatatu itakwea pipa la nne kurudi Bongo kuendelea na maisha.
Prisons iliibana Simba jana na kutoka nayo suluhu katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine matokeo ambayo yameifanya Simba kufikisha pointi 36 na kubaki katika nafasi ya nne huku Yanga ikiwa ya tatu na pointi zake 38, Prisons nayo imesimama nafasi ya 10 ikiwa na pointi 21.
Katika mchezo wa jana, muda mwingi wachezaji walikuwa wanachezeana kibabe na mchezo ulikuwa wa kasi lakini safu za ulinzi za timu zote zilikuwa makini kuondosha hatari zilizoelekezwa kwao.
Katika kipindi cha kwanza Simba ilifanya mashambulizi mengi lakini la maana lilikuwa dakika ya 31 baada ya Amri Kiemba kupiga shuti kali lililotoka nje ya lango. Prisons ilifanya shambulizi kali dakika ya 36 ambapo kipa Yaw Berko alijitahidi kuokoa na mpira ukamponyoka lakini washambuliaji wa Prisons hawakuwa makini kumalizia mpira uliotemwa.
Kipindi cha pili timu zote zilijitahidi kutafuta mabao lakini hakuna upande ulioweza kupata bao hadi dakika 90 zinamalizika. Akizungumza baada ya mchezo huo, nahodha wa Simba, Joseph Owino alisema: “Nashukuru kwa matokeo haya kwani mara nyingi mechi za nje ya Dar es Salaam huwa ngumu kwetu, tunajipanga kwa mechi zijazo.”
Kwa upande wake, nahodha wa Prisons, Lugano Mwangama alisema: “Matokeo haya ni mazuri na Simba wana bahati sidhani kama wangejitahidi kiasi hiki, wana bahati tulikuwa tunawafunga wamejitahidi kuongeza kasi leo.”
Wakati huohuo, JKT Ruvu imeifunga Mtibwa Sugar mabao 2-1 katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa jana Jumapili kwenye Uwanja wa Chamazi Complex, Mbagala, Dar es Salaam.
Mabao ya JKT Ruvu yalifungwa na Kalage Mgunda kwa shuti kali dakika 18 baada ya kupokea pasi ya kichwa ya Idd Mbaga, Amos Mgisa aliifungia JKT Ruvu bao la pili dakika ya 75 akiunganisha pasi ya Mbaga. Vincent Barnabas aliifungia Mtibwa bao pekee dakika ya 70 akimalizia pasi ya Juma Luizio.
Matokeo hayo yameifanya JKT Ruvu kufikisha pointi 25 sawa na Mtibwa lakini imesimama katika nafasi ya tisa na Mtibwa kubaki nafasi ya nane kutokana na kutofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
CHANZO: WANASPOTI

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video