Tuesday, March 11, 2014

SI Azam FC tu inayofanya mambo kisayansi, hata Simba ya Msimbazi na yenyewe imeanza kubadilika.
Azam imeshamsainisha kiraka Owen Kasule wa Uganda tayari kwa msimu ujao lakini Simba kupitia kwa mkurugenzi wake wa ufundi, Moses Bassena inapitia viwanjani kukagua wachezaji wote kwenye timu zote za Ligi Kuu Bara.
Kwa mujibu wa Simba hilo linafanyika ili kuhakikisha wanafanya usajili wa maana na si magarasa kama ilivyokuwa awali kwa kuwafuatilia kwenye mechi zao wanazocheza.
Basena raia wa Uganda aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Napenda kuja kuangalia mechi hizi kwa sababu namjua kila mchezaji hata kama tukimhitaji tunajua uwezo wake uwanjani, kujua kiwango cha mchezaji mwenye ubora ni baada ya kumwona kwenye mechi nne hadi tano na si mchezo mmoja na ndiyo maana napenda kufuatilia kila mchezaji.”
Bosi huyo ambaye aliwahi kuwa kocha wa Simba, amekuwa akibaki Dar es Salaam wakati timu yake ikiwa nje ya mkoa huo au kusafiri mikoa ya jirani kuziangalia timu pinzani kwa lengo la kuzisoma kiufundi na kumuongezea mbinu Logarusic na baadaye kuangalia wachezaji muhimu ambao wanaweza kusajiliwa kwa ajili ya kikosi cha msimu ujao.
CHANZO: MWANASPOTI

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video