Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
WEKUNDU wa Msimbazi Simba SC leo jioni wanacheza
mechi yao ya 22 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam dhidi ya wagosi wa
Kaya, Coastal Union ya jijini Tanga.
Wakiwa tayari wameshashuka dimbani mara 21 na
kujikusanyia pointi 36 katika nafasi ya nne,
Simba chini ya kocha mkuu, Mcroatia, Dravko Logarusic wapo katika
mazingira magumu zaidi ya kupata matokeo ya ushindi.
Simba SC kama vile wameshajitoa katika mbio za
ubingwa na kuwaachia Yanga, Azam na Mbeya city, leo hii watataka kuonesha kuwa
ni wakongwe wa soka la Tanzania.
Loga amekuwa na wakati mgumu tangu aanze kukinoa
kikosi cha Simba mwanzoni mwa mzunguko wa pili akirithi mikoba ya Abdallah
Kibadeni.
Kocha huyo anayesifika kudhibiti nidhamu kwa
wachezaji, amekifanya kikosi cha Simba kuwa cha `tia maji tia maji` kwasababu
leo kinaweza kupata ushindi na kesho
kupoteza mechi.
Utawaweza Coastal Union leo?: Kocha wa Simba, Dravko Logarusic yupo katika wakati mgumu kuipatia mafanikio klabu hiyo msimu huu
Wakati Simba wakiwa na malengo ya kuzoa pointi tatu
kutoka kwa Coastal Union leo ili angalau kusogea juu kwa kufikisha pointi 39,
wagosi wa kaya nao wanahitaji ushindi na kupunguza maumivu ya mabao 4-0 kutoka
kwa Azam FC mechi iliyopita.
Coastal mpaka sasa wapo nafasi ya 7 wakiwa na pointi
26, huku wakisifika kuwa na wachezaji wazuri msimu huu.
Kocha Yusuf Chipo atahitaji kuwapunguzia machungu
wapenzi wa klabu hiyo yenye makazi yake jinni
Tanga.
Coastal Unio wakiwa mazoezini kujiandaa dhidi ya Simba sc
Kutokana na umuhimu wa mechi ya leo kwa Simba na
Coastal Union, mpira unatarajiwa kuwa na
upinzani mkubwa .
Mechi ya mzunguko wa kwanza kule CCM Mkwakwani jijini
Tanga, timu hizi zilishindwa kufungana.
Mechi nyingine yenye mvuto leo hii ni baina ya
vinara, Azam fc dhidi ya JKT Oljoro.
Oljoro wapo nafasi ya 13 wakijikusanyia pointi 15
tu na wapo katika hatari ya kushuka
daraja.
Wataingia kwa lengo la kusaka pointi tatu muhimu,
lakini Azam fc ambao hawajafungwa katika mechi 20 walizocheza, wanahitaji
pointi tatu ili kuwasomesha namba Yanga wanaowafuatia kwa tofauti ya pointi
moja baada ya ushindi wa jana wa mabao 3-0 dhidi ya Rhino Mjini Tabora.
Endapo Azam fc watashinda leo, watafikisha pointi 47
kileleni na kuwaacha Yanga kwa pointi 4,wakati huo huo Yanga watakuwa
wanasubiri mchezo wa machi 26 (jumatano) dhidi ya Tanzania Prisons, uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
Kama Yanga watashinda mechi ijayo na Azam fc
kufungwa leo au kutoka sare basi, Azam
fc atakuwa amepinduliwa kileleni.
Lakini kama Azam fc atashinda leo na Yanga atashinda
jumatano, bado wanajangwani wataendelea kuisoma namba kwa Azam fc.
Mechi nyingine za leo ni Mgambo Shooting dhidi ya
Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, wakati Ruvu Shooting na
Ashanti United zitapimana ubavu kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani
Pwani.
0 comments:
Post a Comment