Thursday, March 13, 2014

Na Baraka Mpenja  , Dar es salaam
0712461976 au 0764302956

WEKUNDU wa Msimbazi Simba wamelaumu timu zinazoingia kwa kukamia wapinzani wao katika mitanange ya lala salama ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014.

Akizungumza na mtandao huu, afisa habari wa Simba Asha Muhaji amesema hali ya kukamiana uwanjani inaharibu ubora wa mpira katika mechi mbalimbali.

“Kuna wakati unaweza kushangaa, mchezaji fulani akawa na kazi ya kumkaba kwa nguvu mshambuliaji wenu. Mfano Amissi Tambwe kwa Simba, badala ya kucheza mpira kwa ufanisi, yeye anacheza kimabavu na kumjeruhi mwenzake. Sasa mpira kama huu hauna maana”. Alisema Asha.

Asha aliongeza kuwa kukamia mechi kwa kucheza mpira mzuri hakuna tatizo kwani kila timu kwa sasa inahitaji ushindi, lakini kukamiana kwa kuumizana si jambo zuri.

“Kuna timu zinahitaji ubingwa au nafasi nzuri za juu, vilevile kuna timu zinakwepa kushuka daraja. Mazingira haya yameifanya ligi iwe ngumu sana. Lakini tatizo ni uchezaji wa ubabe kwa baadhi ya timu. Kuumia ni kawaida katika mpira, lakini kuna mazingira mengine yanatokana na kukamiana”. Alisema Asha.

Pia aliongeza kuwa unaweza kumuona mchezaji akicheza na Simba au Yanga ukajua anafaa, lakini akija kucheza na timu nyingine ndogo anakuwa wa kawaida sana, hivyo inadhihirisha kuwa wanakamia baadhi ya mechi.

Afisa habari huyo alikiri kuwa mzunguko huu wa pili Simba sc hawana mwenendo mzuri sana, ila wanajipanga kuhakikisha wanafanya vizuri mechi za mwisho.

“Simba ni klabu kubwa. Kila mtu anainyooshea kidole kila  inapofanya vibaya. Mpira una matokeo matatu, kufunga, kufungwa na kutoa suluhu au sare. Upepo kwetu umevuma vibaya, lakini itafika wakati mambo yatakwenda vizuri”. Alisema

 Asha.


Nao Wagonga nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya City walisema kukamiana si jambo geni katika mpira duniani kote.

Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Maka Mwalwisyi alisema kuwa kuwepo kwa ligi ya ushindani ni jambo jema ambalo wadau na mashabiki wa soka wanatakiwa kufurahia.

“Siku za nyuma matokeo yalikuwa yanatabirika kirahisi hasa Simba au Yanga zinapoingia uwanjani, lakini kwa sasa zimekuja timu nyingi zenye ushindani. Ligi yoyote ile inatakiwa kuwa hivi”. Alisema Maka.

Akizungumzia suala la kukamiana katika mechi za ligi hiyo, kocha huyo alisema ni jambo la kawaida katika soka, lakini akaeleza kuwa kuna kukamiana kwa aina mbili.

Moja; timu inakamia kutafuta ushindi kwa kushindana dakika zote za mchezo, lakini wanacheza mpira wa ushindani bila kufanya madhambi (rafu) kwa wapinzani wao. Aina hii ya kukamiana ni nzuri katika soka.

Pili; kuna kukamia kwa kufanya rafu kwa wapinzani. Aina hii lazima ipingwe nguvu zote kwani inaharibu ubora wa mechi.

Ikizungumzia uhalisia wa ligi kuu kwasasa, Maka alisema hadhani kama timu zinakamiana kwa kucheza rafu, japokuwa kuna baadhi ya matukio yanaweza kukufanya uamini hivyo.

“Sijawahi kusikia kwenye mechi moja zikatoka kadi nyekundu nne au tatu msimu huu. Hii inaonesha kuwa timu zinakamiana kwa kutafuta ushindi. Hivyo naamini suala la kujadili si kukamiana, bali ni ushindani wa ligi kuwa mkubwa”. Alisema Maka.

Akizungumzia wachezaji wao wawili waliojeruhiwa katika mchezo wa wiki iliyopita uwanja wa Sokoine dhidi ya maafande wa JWTZ, Rhino Rnagers, Mwagane Yeya na Richard Peter, Maka alisema wanaendelea vizuri na matibabu.

“Mwagane anaweza kutumika katika mchezo ujao dhidi ya JKT Ruvu Chamazi, lakini Peter bado hajawa fiti kwa sasa na yupo chini ya uangalizi makini wa daktari wetu. Sidhani kama ataweza kurudi katika hali yake kwa haraka”. Alisema Maka.

Mbeya City wapo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 39  nyuma ya Azam fc wenye pointi 40 kileleni.

Nafasi ya tatu wapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Dar Young Africans wakiwa na pointi 38, lakini wana michezo mkononi.


Wekundu wa Msimbazi Simba wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi 36.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video