Thursday, March 13, 2014

Katibu Mkuu wa Simba,Ezekiel Kamwaga.
........................................

Uongozi  wa Klabu ya Simba umelituhumu Shirikisho la Soka nchini (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) kuhujumu mapato yatokanayo na viingilio vya milangoni kwenye viwanja mbalimbali vinavyotumika kwa mashindano yanayosimamiwa na vyombo hivyo vya soka nchini.

Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa 'kuna watu wa mpira' ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakizihujumu klabu kwa kutengeneza tiketi za bandia na kuziuza wakati wa mechi huku pesa zote zikiishia kwenye mifuko yao.

Kamwaga alidai kuwa Simba iliibiwa sehemu kubwa ya mapato ya mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons iliyochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya.

"Uwanja wa Sokoine ulionekana umefurika pande zote lakini ripoti ya mapato yaliyopatikana ni Sh. milioni 30 tu, Klabu ya Simba imechoka kuvumilia hujuma hizi. Mechi yetu iliyotangulia hapa dhidi ya Mbeya City iliingiza zaidi ya Sh. milioni 100 na uwanja ulikuwa umefurika kama ilivyokuwa Jumapili, nashangaa kuambiwa mapato ni Sh. 

milioni 30 huku kila klabu ikiambulia Sh. milioni saba ambazo hazitoshi hata nauli ya kusafirisha wachezaji wetu kutoka Mbeya hadi Dar es Salaam," alisema Kamwaga.

Kiingilio katika mechi hiyo iliyomalizika kwa suluhu kilikuwa Sh. 5,000 na Kamwaga alisema wameelezwa kwamba watazamaji waliokata tiketi halali ni watu 6,336 tu kati ya tiketi 20,000 zilizoandaliwa na kupigwa mihuri.

Kadhalika alisema kilikamatwa kitabu cha tiketi 500 ambazo zilikuwa hazijagongwa muhuri katika mechi yao iliyopita dhidi ya Mbeya City kwenye uwanja huo. 

Alisema uongozi wa Simba unaamini tatizo hilo litamalizwa na mfumo wa tiketi za elektroniki ambao TFF imeusitisha ili kurekebisha kasoro zilizojitokeza baada ya kuanza kutumika katika baadhi ya viwanja katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.

Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine una uwezo wa kuingiza watu 21,000 kwa mujibu wa Silas Mwakibinga, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, lakini baadhi ya viongozi wa Chama cha Soka mkoani Mbeya (Mrefa) wanadai kuwa una uwezo wa kuingiza watu 30,000.

Alipoulizwa kuhusu madai ya Simba, Mwakibinga alisema: "Kabla ya mechi viongozi wa Simba na Prisons walikutana kuhakiki tiketi, lakini Uwanja wa Sokoine una matatizo ya watu kupita njia za panya na baadhi ya wasimamizi wamekuwa wakiingiza watu kinyemela."

"Tunasubiri wenzetu CRDB (walioshinda tenda ya tiketi za elektroniki) warekebishe upungufu uliojitokeza katika tiketi za elektroniki ambazo tunaamini ndiyo suluhisho la matatizo hayo. Wakisharekebisha, tutaanza kuzitumia mara moja."

MREFA WANENA
Hata hivyo, katika mahojiano maalum na gazeti hili jijini Mbeya wiki iliyopita, uongozi wa Mrefa ulidai kuwa kuna mtandao mkubwa wa wahujumu wa mapato ya mechi za soka unaohusisha pia baadhi ya watendaji wa TFF.

"Ligi Kuu ni mali ya TFF, sisi (Mrefa) tunasaidia kusimamia mechi za ligi hiyo katika masuala ya usalama, mapokezi ya wasimamizi wa mechi husika lakini tiketi huandaliwa na Bodi ya Ligi Kuu.

Tunashangaa kunapoibuka tiketi za ziada ambazo hazijapigwa mihuri katika baadhi ya mechi zinazochezwa jijini hapa. Tunaamini TFF na bodi hiyo wanawajua wanaojihusisha na suala hilo," alisema mmoja wa viongozi wa Mrefa ambaye aliomba hifadhi ya jina lake.

TFF WANENA
Boniface Wambura, Ofisa Habari wa TFF, aliiambia NIPASHE jijini Dar es Salaam jana kuwa bado hawajapelekewa rasmi malalamiko ya klabu ya Simba.

"Mpaka sasa (jana saa 11:09 jioni) hatujapata barua ya Simba kuhusu suala hilo, tutatoa ufafanuzi baada ya kupata malalamiko hayo rasmi," alisema Wambura huku akisisitiza kuwa uwezo wa viwanja usipimwe kwa macho. 

Hiyo si mara ya kwanza uongozi wa Simba kulalamika juu ya hujuma za mapato ya timu za klabu na timu za taifa zinazofanywa na baadhi ya wadau wa soka nchini wakiwamo watendaji wa TFF.

Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu, Simba kupitia kwa Kamwaga walidai kuwa klabu yao ilikumbana na hujuma za mapato katika mechi zake zikiwamo mbili za mikoani walizotoka sare ya 2-2 dhidi ya Rhino Rangers mjini Tabora Agosti 24, mwa jana kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya Oljoro JKT jijini Arusha Agosti 28, mwaka jana.

"Mechi zetu Tabora na Arusha 'tumepigwa' (tumehujumiwa) kiasi kikubwa cha pesa... Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ulikuwa umefurika kila upande, lakini baada ya ukaguzi wa vitabu vya tiketi kufanyika, ikaonekana watu waliolipia tiketi halali walikuwa 12,981 tu.

Arusha pia tukapigwa, ni tatizo kubwa kwa soka la Tanzania," alisema Kamwaga katika mahojiano maalum na NIPASHE Septemba mwaka jana jijini Dar es Salaam.

 "Kuna watu wengi wanakamatwa na tiketi za ziada na bandia katika mechi za timu za klabu na timu za taifa. Tulishasema waanze kutumia tiketi za elektroniki lakini suala hilo linapigwa danadana kila mara ilhali klabu zinaumizwa kimapato."

Katibu wa Chama cha Soka Tabora (Tarefa), Fateh Remtura na Katibu wa Chama cha Soka Arusha (ARFA), Adam Brown waliunga mkono madai ya Kamwaga na kwamba wao pia walishangazwa na idadi ndogo ya tiketi halali zilizonunuliwa katika mechi za Rhino Rangers na Oljoro JKT dhidi ya Simba mzunguko wa kwanza.

"Sisi (Tarefa) tulihakiki vitabu vyote tukiwa viongozi wa Simba na Rhino na wawakilishi wa TFF, tukaona tiketi zilizokuwa zimenunuliwa ni 12,981. Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi uliojengwa 1987 una uwezo wa kuchukua watu 30,000 na ulikuwa umefurika, huwa tunasikia kuna watu huuza tiketi bandia. Ninyi waandishi wa habari mtusaidie kuwafichua," alisema Remtura.

"Mechi ya Oljoro JKT dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wenye uwezo wa kuingiza watu 15,000 iliingiza Sh. milioni 38 za mauzo ya tiketi halali 7,340. Hata hivyo, uwanja huo ulikuwa umefurika watu kila upande huku wengine wakilazimika kusimama sehemu ya chini ya jukwaa kuu," alisema Brown.

MASHABIKI MBEYA
Baadhi ya mashabiki waliozungumza na NIPASHE jijini Mbeya wiki iliyopita walidai kuuziwa tiketi zisizo na mihuri katika mechi za ligi kuu zinazochezwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini humo.

"Tiketi zimekuwa zikichelewa kuanza kuuzwa hasa kunapokuja timu za Simba na Yanga kucheza na timu za mkoa wetu. Wakati mwingine, hasa kunapokuwa na mechi kubwa, huwa tunauziwa tiketi zisizo na mihuri," alisema Michael Kasyupa, mmoja wa mashabiki wa soka mkoni Mbeya.

RIPOTI YA KAMATI YA TENGA
Mei 2011 aliyekuwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, kwa mamlaka aliyokuwa nayo kwa mujibu wa Katiba ya shirikisho hilo lenye mamlaka ya juu kisoka nchini, aliunda Kamati Maalum ya Kudhibiti na Kuboresha Mapato ya TFF iliyokuwa na wajumbe nane kuchunguza mwenendo wa shirikisho hilo kimapato na matumizi.

Ukurasa wa 29 wa ripoti ya kamati hiyo yenye jumla ya kurasa 95 na viambatanisho tisa unasema: “Baadhi ya watendaji ndani ya TFF wanajihusisha na kuhujumu mapato kwa kuchapisha tiketi za ziada na kuziuza kwanza.”

“Kuna tiketi nyingi za kugushi/ bandia zinazotengezwa kwa ushirikiano kati ya baadhi ya viongozi wa soka na wapenzi wa mpira wa miguu. Viongozi hawa ni wale walioko madarakani,” inaeleza zaidi ripoti hiyo ukurasa wa 30.

Baada ya kubaini upungufu huo, kamati hiyo ambayo Tenga alikuwa mwenyekiti, inashauri katika ukurasa wa 31 kwamba, TFF iachane na mfumo wa tiketi za kawaida na kuanza kutumia tiketi za elektroniki.

TFF ilianza kufanyia kazi pendekezo la kamati hiyo iliyokuwa na wajumbe 'wazito' wakiwamo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova na mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali Mstaafu Idd Kipingu, kwa kutangaza tenda ambayo CRDB walishinda kutengeneza tiketi hizo ambazo Tenga aliagiza zianze kutumika katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara msimu uliopita.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video