Rais Dkt. Jakaya Kikwete akimkaribisha Ikulu kwa mazungumzo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mheshimiwa Dkt. Frank-Walter Steinmeier. Waziri huyo aliwasili nchini tarehe 25.3.2014 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mheshimiwa Dkt. Frank-Walter Steinmeier na baadhi ya viongozi aliofuatana nao wakati walipomtembelea Rais Dkt. Kikwete huko Ikulu tarehe 25.3.2014. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatana na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Dkt. Frank- Walter Steinmeier wakitoka nje kwenda kuona sehemu ya jengo la ikulu lililojengwa na Wajerumani wakati wakiitawala Tanganyika. Wengine waliofuatana nao ni Balozi wa Tanzania huko Ujerumani Mheshimiwa Phillip Marmon na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Dorah Msechu.Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwaonyesha wageni wake jengo la ikulu sehemu iliyojengwa na Wajerumani (jengo halionekani pichani) mara baada ya kufanya mazungumzo na ugeni huo.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
0 comments:
Post a Comment