Ni siku 100 tu, ni vigumu kuamini kuwa iko karibu. Inaonekana kama jana tu kwamba Brazil imethibitishwa kuwa muandaaji wa FIFA World Cup 2014. Nakumbuka msisimko niliohisi na kuona kuwa nchi yangu inaenda kwenye hatua muhimu ya mpira katika Dunia hii.
Hata ingawa mimi sitakuwa uwanjani, lakini nimeanza kupata vipepeo tumboni kama ambavyo nilikuwa nikikaribia mechi kubwa. Baada ya yote kumalizika FIFA World Cup, itakuwa ni ya aina ya mwisho kwa Brazil, tofauti na kujitangaza yenyewe kimataifa. Uangalizi utakuwa juu yetu na ni nafasi kubwa kwetu kwa kuionyesha Dunia umuhimu kuhusu Brazil na watu wa Kibrazil walivyo.
Wakati wa Kombe la Dunia la Olimpiki 2016 itakayofanyika Brazil, tutakuwa na nafasi ya kuionyesha Dunia jinsi tunavyo penda michezo na vilevile tulivyo na nguvu katika uchumi wetu. Brazil ni kiongozi mkubwa Duniani kiteknolojia na kiongozi mkubwa wa uzalishaji wa Nyama, madini na mzalishaji mkubwa wa soya duniani. Ni karibu sasa maelfu ya watalii na waandishi wa kigeni watafika kwenye mlango wetu ulio wazi kujionea na kugundua uhalisia wa Wabrazili.
Ingawa Brazili ni nchi kubwa kijamii, lakini tumefanya mambo mengi ya kukabiliana na matatizo katika miaka ya hivi karibuni. Tuna utaifa tofauti lakini tuna umoja mzuri kijamii na kimaendeleo katika ubunifu wa juu. Ni nchi iliyojaliwa watu wenye uwezo mkubwa kiakili na inawatu wengi wenye vipaji vikubwa katika michezo kama Neymar anavyocheza na maajabu yake ya kuchezea mpira . Vilevile mziki wa Tom Jobim na sayansi aliyoipata kutoka kwa Miguel Nicolelis, kama utafiti waliofanya na kupata matumaini kuwa siku moja mifupa ya binadamu inaweza kutembea tena.
Brazili ni nchi nzuri sana, na ni nchi iliyobarikiwa kuwa na hali ya asili nzuri. Watalii wote watakaofika Brazil wakati wa Kombe la Dunia wajiandae kukutana na hali ambayo hawataisahau na hawajawahi kuiona. Vilevile watafurahia kutembelea fukwe za kusini na kujionea misitu na mto wa Amazon, milima katika mji wa Rio de Janeiro ambayo ni sehemu muhimu sana kwa watalii. Naamini kila mtalii ataondoka Brazil akiwa na kumbukumbu nzuri katika maisha yake yote.
Brazili ni nchi nzuri na ya furaha sana. Tunawakaribisha watalii wote katika Kombe la Dunia kwa mikono yote miwili na hadi tutakapo anza kufanya kazi.
Kwa mwaka 2014 FIFA World Cup taasisi za mitaa na uongozi wa bodi ya wanachama, nimeridhika mwenyewe kwa kuona uwezo wao na uzoefu walionao wa kusimamia tamasha kubwa hili. Ndani ya miji yote 12 itakayofanyika mashindano haya, nimeshuhudia maelfu ya watu wakihakikisha kuwa mashindano ya Kombe la Dunia yanafanyika katika hali nzuri.
Tumekumbana na vikwazo vigumu katika maandalizi ya Kombe la Shirikisho la FIFA mwaka jana ambapo tulikuwa wenyeji. Hayo siyo maoni yangu tu bali maoni ya washabiki wote wanahabari, na vilevile Raisi wa FIFA Joseph S. Blatter.
Chini ya miezi sita baadae kwa mafanikio tuliandaa tukio la changamoto nyingine. Droo ya mwisho katika mji wa Costa do Sauipe Bahia. Na tulipogundua ni katika miji ipi michezo itakapochezewa timu za mataifa 32 ambazo zitapinga mashindano zilijadiliana mipango yao ya kiutekelezaji na uanachama wa LOC, FIFA na serikali ya Brazil. Kubadilishana huku kwa mawazo na maoni baina ya waandaaji wa timu za taifa ni mchakato unaoendelea, na tukio jingine muhimu la warsha ya timu za taifa mjini Costao do Santinho katika mji wa Florianopolis uliofanyika mwezi uliopita. Mada zikiwa kama vile , usalama, usafiri na jinsi timu zitakavyohudumiwa vilijadiliwa kwa undani.
Hivi sasa tuko nyumbani moja kwa moja , toka mwanzo wa mwaka viwanja viwili vya mpira vimefunguliwa ambavyo ni Arena Amazonas, Arena da Baixada, Arena Pantanal na Arena Corinthians, ambavyo karibia viko tayari. Wakati Kombe la dunia likianza viwanja vyote vitakuwa vimeshafanyiwa matukio ya majaribio. Haya yote ni muhimu sana ili waandaaji waweze kufanya marekebisho ya mwisho katika mipango yao.
Hatuna muda mwingi wa kutosha mpaka mashindano yatakapoanza, na wachezaji wakubwa katika sayari kwenda kifua mbele kama, Messi, Christiano Ronaldo, Iniesta, Neymar…..siwezi kungojea. Ninawatarajia nchini Brazil. Tutaonana katika Kombe la dunia.
0 comments:
Post a Comment