Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
0712461976 au 0764302956
MCHEZAJI nyota wa Asernal, Alex Oxlade-Chamberlain anaamini kuwa klabu yake itasonga mbele katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA Champions League) katika mchezo ya marudiano hapo kesho, licha ya kupigwa mabao 2-0 na mabingwa watetezi, Bayern Munich mchezo wa kwanza uwanja wa Emirates jijini London.
Kiungo huyo amejenga imai hiyo kwa kutumia uzoefu wa msimu uliopita ambapo washika bunduki hao walishinda mabao 2-0 katika dimba la Allianz Arena baada ya kupoteza mchezo wa kwanza katika dimba lao kwa mabao 3-1, hivyo anaamini kwa asilimia 100 kuwa kitu hicho kinaweza kujirudia.
Asernal wapo katika furaha ya kuwabamiza Everton mabao 4-1 katika mchezo wa kombe la FA na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambapo watakabiliana na Wigan uwanja wa Wembley, hivyo kuwa na matumaini ya kutwaa kombe la kwanza tangu mwaka 2005.
Alex Oxlade-Chamberlain akipanda ndege wakati wakielekea uwanja wa Luton Airport jijini Munich nchini Ujerumani
Mchezo wa marudiano utakaopigwa kesho utaamua hatima ya Asernal katika michuano ya kimataifa barani Ulaya. Kama watatupwa nje basi watabaki katika kinyang`anyiro cha ubingwa wa ligi kuu nchini England ambapo wapo katika ratiba ngumu ya kuwavaa ugenini Tottenham na Chelsea kabla ya kuwakaribisha nyumbani, Manchester City machi 29.
Bayern Munich wameweka rekodi katika ligi ya Bundesliga baada ya kushinda michezo 16 mfululizo na mchezo wa mwisho waliwafunga mabao 6-1 Wolfsburg, na sasa kikosi cha Pep Guardiola kipo mbele kwa pointi 20 dhidi ya wapinzani wao wa karibu, Borussia Dortmund huku wakibakiwa na mechi 10.
Asernal watamkosa kiungo wao, Muingereza Jack Wilshere ambaye yupo nje kwa wiki sita baada ya kuvunjika mguu, wakati huo huo mlinda mlango wao namba moja. Wojciech Szczesny ataukosa mchezo huo kufuatia kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo wa kwanza.
Mholanza, Oxlade-Chamberlain alisisitiza kuwa bado nafasi ipo kama Asernal wataendeleza rekodi ya ushindi wa mabao 2-0 katika dimba la Allianz Arena, msimu wa mwaka jana. Kikubwa watafute mabao tu.
Tayari kwa safari: Mesut Ozil, Mathieu Flamini na Lukas Podolski wakielekea uwanja wa ndege
Kazi tu: Mathieu Flamini na Laurent Koscielny wakiwa ndani ya ndege kuelekea Munich
“Nsdiyo, asilimia 100 tunaweza kushinda. Msimu uliopita tulifungwa 3-1 nyumbani-kila mtu aliona hatuwezi, lakini tuliweza kuwafunga kwao 2-0″. Alisema kiungo huyo.
“Tutaweza kufanya vizuri ukizingatia tulicheza kwa kiwango cha juu jumamosi dhidi ya Everton”.
Katika soka, vitu vingi vinaweza kutokea. Tunajua wanajua kazi haijaisha, hata sisi tunajua kazi haijaisha”. Aliongeza.
Kazi imenza: Wachezaji wa Arsenal, Mesut Ozil na Lukas Podolski wakiwasili mazoezi huku wakionekana hawana wasiwasi.
Wagumu wa ngome: Per Mertesacker na Laurent Koscielny wakiwasili katika mazoezi ya kuwakabili Bayern Munich
Wachezaji wa Arsenal wakipasha jijini London katika dimba la Colney kabla ya kuwasili Munich
0 comments:
Post a Comment