Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damian Lubuva akifafanua jambo kwa msisitizo kuhusia na maandalizi ya mwisho ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, unaotarajiwa kufanyika Machi 16, mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya Siasa,vyombo vya usalama na wadau wengine
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo,kuhusu uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga katika kikao cha pamoja na vyama vilivyosimamisha wagombea kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo ulioko Halmashauri ya wilaya ya Iringa Vijijini.Uchaguzi wa Jimbo hilo unatarajiwa kufanyika Machi 16.Ambapo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ameeleza kuwa idadi ya wapiga kura jumla yao ni 71,765.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damian Lubuva akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid kwenye mkutano uliohusu kupeana taarifa ya maandalizi ya mwisho ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga,unaotarajiwa kufanyika Machi 16,mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya Siasa,vyombo vya usalama na wadau wengine,mkutano huo umefanyika leo asubuhi kwenye ukumbi wa Siasa ni Kilimo zilizomo ndani ya Ofisi za Halmashauri Wilaya ya Iringa.
Mkurugenzi wa Oparesheni wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi wa Kalenga,Benson Kigaila wakisalimiana kwa furaha na Mmratibu wa kampeni CCM Kalenga Miraji Mtaturu.
Mkurugenzi wa Oparesheni wa chama cha demokrasia na maendeleo katika uchaguzi wa Kalenga Benson Kigaila aliyesimama kwa nyuma akizungumza na mratibu wa kampeni ccm Kalenga Miraj Mtaturu kulia kwake ni mratibu wa uchaguzi wa ccm Taifa Edwin Millinga.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akijadiliana jambo na Afisa msajili msaidizi wa vyama vya siasa Sisty Nyahoza.
Wanahabari wakijadiliana jambo.
Baadhi ya Wanahabari wakiwa katika kikao cha Tume ya Uchaguzi n Vyama vya siasa na baadhi ya wadau wa usalama.
PICHA NA MICHZUIJR. MICHUZI MEDIA GROUP-IRNGA
0 comments:
Post a Comment