Thursday, March 13, 2014

Mwimbaji-wa-muziki-wa-injili-Boniface-Mwaitege-akiimba-katika-Tamasha-la-Krismas-lililofanyika-Uwanja-wa-Jamhuri-Mjini-Morogoro.Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kimelibariki Tamasha la Pasaka  na kutoa wito kwa mashabiki mbalimbali wa muziki huo hapa nchini kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo linalotarajia kuanza Aprili 20 jijini Dar es Salaam.
Chamuita inatambua mchango wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama ambaye ni muandaaji wa matamasha ya Pasaka na Krismasi kwa kutambua mchango wake wa kufanikisha matamasha  hayo, kwenye tamasha litakalofanyika jijini Dar es Salaam watamkabidhi cheti cha kutambua mchango wake, Msama.
Akizungumza na mwandishi wa makala hii, Mwenyekiti wa Chamuita, Addo Novemba anasema Msama ni mmoja wa mifabo ya kuigwa kwa jamii kutokana na kufanikisha maendeleo ya muziki huo hapa nchini hasa kuwanyanyua waimbaji chipukizi.
Novemba anasema kwenye tamasha la mwaka huu watashiriki kikamilifu kwa sababu wanatambua anayoyafanya Msama kwa kumtumikia Mungu ipasavyo.
Novemba anasema utekelezaji wao wa tamasha la mwaka huu watakuwa bega kwa bega na Msama katika ufanikishaji wa tamasha hilo lenye lengo la kuzungumza na Mungu kupitia waimbaji  na viongozi mbalimbali wa Tanzania na nje.
Aidha Novemba anatoa wito kwa Watanzania kuipenda nchi yao hasa kupitia kauli mbiu ya Uzalendo Kwanza, Haki huinua Taifa, hivyo Watanzania wajiandae kuipenda nchi yao zaidi ya wanavyoipenda.
“Watanzania Tamasha la Pasaka ni la Msama hivyo ni la kwetu sote, walipende kwa sababu ni lao kwa kujitokeza kwa wingi kwenye matamasha yanayoandaliwa naye.”
Novemba anasema Msama anaepusha mambo mengi yanayomchukiza Mungu kwa kuandaa matamasha ya kumrudia Mungu kwa kutenda mema ambayo yatampendeza Mungu.
“Msama anasaidia kuachana na mambo  mabaya yanayomchukiza Mungu kama ulevi wa kupindukia ama kuzungumzia mambo ya umbea na badala yake wajitokeze kwenye matamasha ya Pasaka na Krismasi,” alisema Novemba.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video