Picha na Bin Zubeiry
KLABU ya Yanga SC imeipa siku tano Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar
es Salaam kutoa idhini ya kujenga Uwanja wa kisasa katika eneo la
Jangwani mjini hapa, vinginevyo wataandamana kushinikiza suala hilo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu hiyo makutano ya
mitaa ya Jangwani na Twiga mjini hapa mchana wa leo, Katibu wa Baraza
la Wazee la Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amesema wamebaini wanawekewa
vikwazo na baadhi ya madiwani wa Manispaa hiyo.
Kumsikia Mzee Akilimali bofya hapa chini
0 comments:
Post a Comment