Baada ya suluhu ya leo na Tanzania Prisons, katika uwanja wa sokoine jijini Mbeya, Simba wamekiri ugumu wa mechi hiyo.
Akizungumza kutoka Mbeya, afisa habari wa Simba,
Asha Muhaji amesema kuwa mchezo ulikuwa mgumu sana kwao kulingana na mazingira
ya wapinzani wao.
“Simba tunahitaji kufanya vizuri ili tukae nafasi
nzuri katika msimamo, wakati Prisons wao wanahitaji pointi ili kuendelea
kujinusuru kushuka daraja. Kwa mazingira hayo ndio maana mechi ilikuwa ngumu
kwa timu zote”. Alisema Asha.
Aidha aliwaomba mashabiki wa Simba kuendelea kuiunga
mkono klabu yao kwani bado wanazo mechi mkokoni na wanatarajia kufanya vizuri.
Kumsikiliza Asha Muhaji akiongea na mtandao huu kutoka Mbeya leo hii bofya hapa chini.
0 comments:
Post a Comment