Thursday, March 13, 2014


DSC_8730
Alex Msama
Na Mwandishi Wetu
 
TAMASHA la Pasaka mwaka huu linatarajiwa kufikisha miaka 14 tangu kuanzishwa kwake na kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam.
Tangu kuanzishwa kwa tamasha hilo Watanzania wameweza kujumuika pamoja siku ya sikukuu hiyo ya kufa na kufufuka kwa Kristo Yesu kwa kutumbuizwa na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
Umaarufu wa matamasha hayo umetokana na waandaaji wake kuweza kuyaandaa kwa ubunifu mkubwa na umakini ambapo tamasha hilo limekuwa kivutio kwa watu mbalimbali huku mikoa mingi nchini ikipigania tamasha hilo kufanyika mikoa hiyo.
Pamoja na Kampuni ya Msama Promotions kuandaa tamasha la Pasaka kila mwaka, kampuni hiyo pia ni waandaaji wa tamasha la Krismasi ambalo lilianza kufanyika mwaka jana ikiwa ni mara yake ya kwanza.
Hata hivyo Mwenyekiti wa matamasha hayo, Alex Msama anabainisha wazi kuwa matamasha hayo yatakuwa ya kudumu na yenye lengo moja la kuhamasisha amani, umoja na mshikamano nchini.
Hata hivyo anaeleza kuwa kauli mbiu ya tamasha la Pasaka mwaka huu ni ‘Uzalendo kwanza, haki huinua taifa’. Kauli mbiu hii ni kwa ajili ya kuhamasisha na kuchochea juhudi za maendeleo nchini, kwa kizazi kilichopo na kijacho.
Katika kutimiza miaka 14 ya Tamasha la Pasaka, kampuni ya Msama Promotions imeeleza kujiandaa vya kutosha katika kuhakikisha tamasha hilo linafana na kuzidi kuwa bora kutokana na uzoefu wa kuandaa matamasha hayo nchini kuongezeka siku hadi suku.
Pamoja na kujiandaa vya kutosha katika tamasha la mwaka huu, kampuni imeweza kubuni utaratibu wa kufanya kile mashabiki wanahitaji kwa kutoa nafasi kwa mashabiki kujichagulia waimbaji wanaoamini kuwa watawaburudisha zaidi.
“Mwaka huu tumeamua kuwaacha mashabiki wajichagulie waimbaji, hivyo tumeweka utaratibu wa kupiga kura ambapo kwa kutumia simu za mkononi, unaenda kwenye sehemu ya ujumbe mfupi wa maandishi, unaandika jina la msanii, mgeni rasmi na mkoa unachokitaka kwa nyakati tofauti, kisha unatuma ujumbe huo kwenda namba 15327, kisha tutaangalia waliopigiwa kura nyingi nao wataweza kupata nafasi ya kuwemo katika tamasha letu la mwaka huu.”
Pamoja na juhudi hizo za uandaaji wa tamasha hilo nchini, kampuni hiyo imeweza kurudisha shukrani zake kwa Watanzania kila lifanyikapo tamasha hilo nchini kwa kuhakikisha inakuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii isiyojiweza ili kuweza kujimudu kimaisha.
Mkakati mkubwa wa kampuni ni kujenga kituo cha kisasa kwa ajili ya watu wenye uhitaji maalum kitakachojengwa eneo la Pugu kitakachokuwa na jina la Jakaya Mrisho Kikwete rafiki wa wasiojiweza ambacho kitasaidia kuwaunganisha watu wenye uhitaji maalum ili waweze kupata uangalizi wa karibu ikiwa ni pamoja na kuonyeshwa upendo.
Katika maandalizi ya Tamasha la pasaka linalotarajiwa kuanza Aprili 20 jijini Dar es Salaam litaweza kujumuisha wasanii mbalimbali wa nyimbo za injili kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika huku waimbaji kutoka nchini Tanzania ambao watakutana na changamoto kubwa na kujifunza kutoka kwa wenzao kutoka nje ya nchi.
Kupitia mapato yanayopatikana kupitia Tamasha la Pasaka husaidia wenye uhitaji maalum kama wajane, walemavu, yatima na wengine wenye uhitaji maalum katika maeneo mbalimbali kama ada za shule na kwingineko.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video