Thursday, March 13, 2014

wanafunzi1
Na Gladness Mushi , Karatu
Mkuu wa wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha Daudi Mtibenda ameviagiza vyuo vyote vya ufundi katika Wilaya hiyo kuanza upelelezi rasmi kwa watoto wa kike hasa wale ambao wanapata mimba wakiwa katika Umri mdogo kwani kwa sasa jamii inamitazamo mibaya dhidi ya vyuo vya ufundi hasa katika maeneo ya vijijini
Amedai kuwa kwa kufanya hivyo kutaweza kuwasaidia hata wamiliki wa vyuo hivyo vya ufundi kufikia malengo yao ya kuwakomboa watoto wa kike katika suala zima la mimba za utotoni.
Mtibenda aliyasema hayo wakati akiongea na wanawake kutoka katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ambao wanalelewa na chuo cha ufundi cha Lake eyasi Wilayani humo mapema wiki hii.
Alidai kuwa kwa sasa asilimia kubwa ya wanafunzi ambao wanapata mimba wakiwa katika masomo yao wanalazimika kukimbizwa katika vyuo vya ufundi bila kujali kuwa maono yao ya hapo baadaye yatakwua yameharibika vibaya jambo ambalo nalo linatakiwa kuchukuliwa hatua kubwa
Alifafanua kuwa asilimia kubwa ya vyuo vya ufundi hapa nchini vimeonekana kama madampo ya kuwalea waliopata ujauzito kwenye umri mdogo na hivyo kwa sasa ni jukumu la kila mmiliki wa chuo naye kuanza kutafuta namna ya kufanya tathimini juu ya matatizo ya mimba.
“mimi napigwa vita sana hapa karatu kwa kuwa huwa nasema kweli na kuanzia sasa naagiza wamiliki wa hivi vyuo vya ufundi kuhakikisha kuwa mnakuwa nayi ni wafuatiliaji wa hizi mimba za utotoni msikubali kutupiwa tu mzigo kwani hata watoto wenyewe nao wanajua wakipata mimba sekondari watakimbilia kwenu tukifanya hivyo tutakuwa tunadumaza hili taifa letu”aliongeza Mtimbenda.
Katika hatua nyingine Mkurrugenzi mtendaji wa Chuo hicho cha ufundi cha Lake Eyasi Bi Ligtness Bayo alidai kuwa chuo hicho kimekuwa ni mkoombozi mkubwa sana kwa watoto wa kike lakini pia hata wanawake ambao wanaishi katik mazingira magumu
Alidai kuwa mpaka sasa zaidi ya wanawake 100 kutoka katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo ya Karatu wameweza kufaidia na elimu itolewayo chuoni hapo na hivyo pia hata wengine nao wameweza kujiajiri wenyewe
Awali alidai kuwa chuo hicho kima mikakatyi ya kujenga vituo vingine ambavyo navyo vitatumika kama vyuo kwa ajili ya kuweza kuwasaidia wanawake wa vijijini pamoja na watoto wa kike ambao wamekatizwa masomo.
“mpaka sasa tumeshaona faida kubwa sana ya kuweza kumsaidia mtoto wa kike lakini pia hata mama ambaye anatoke a katika maazingira magumu na kwa maana hiyo basi tumefanya utaratibu wa kuanza kuomba ardhi kwa wananchi ili tuweze kujenga tena vyuo vingine vitatu katika kata hii hii ya Mangola’aliongeza Ligtness
Alimalizia kwa kuiomba Serikali nayo kuweza kuangalia changamoto mbalimbali ambazo zipo kwenye Kituo hicho ambacho ni nkama chuo cha wanawake ili nacho kiweze kufikia malengo mbaimbali ya kuwakomboa wanawake kwa ujumla.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video