Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania, mapema mwaka huu umeanzisha mradi wa urasimishaji wa mashamba ya wakulima wadogo wa zao la miwa wilaya za Kilombero na Kilosa mkoani Morogoro.
Aidha taarifa ilieleza kuwa Mpango huo utahusisha vijiji vinne vya Ruhembe, Kidogobasi,Kihelezo, Kitete-Msindazi na vingine sita kutoka Wilaya ya Kilombero Mkula ,msolwa ujamaa, Katurukila, Sonjo, Sole na Magombera.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam Jumla ya hati miliki 8,902 za kimila zimeandaliwa 3,679 zimesajiliwa na nyingine 2142 zimetolewa kwa wamiliki wa wilaya za Njombe, Mufindi na Rungwe katika kutekeleza zoezi hilo la urasimishaji lilioanza Novemba 2011.
Utekelezaji huo ni wa awamu ya nne unaofanywa na MKURUBITA kwa lengo la kukuza mtaji na utawala bora ili kuwawezesha wananchi kuinua mapato yao kwa kupunguza umaskini kwa manufaa yao.
Pia MKURABITA kwa kushirikiana na wadau wake imetoa wito kwa wakulima wa miwa Kilosa na Kilombero kuonana na uongozi wa vyama vya wakulima wa miwa kutoka Ruhembe, Kidatu na Msolwa kwa ajili ya kuthibitisha umiliki wa mashamba.
MKURABITA imeandaa mafunzo kwa ajili ya mipango na michanganuo ya biashara kwa kuwaunganisha wakulima na Taasisi za mitaji na mikopo , baada ya kukamiliksha zoezi la mchakato wa urasimishaji wilayani Kilosa na Kilombero.
0 comments:
Post a Comment