Tuesday, March 11, 2014

Dar es Salaam. Kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime amekwepa mzigo wa lawama kwa kusema wachezaji wake ndiyo wanayo majibu ya swali kwa nini mwenendo wa timu hiyo hauridhishi.
Mwishoni mwa wiki, Mtibwa Sugar iliogelea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa timu ya JKT Ruvu katika pambano lililopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Kipigo hicho cha mwishoni mwa wiki ni mwendelezo wa matokeo mabaya ya timu hiyo yenye maskani yake Manungu mkoani Morogoro, kwani haijashinda mchezo wowote ugenini tangu mzunguko wa pili ulipozinduliwa Januari 25 mwaka huu.
Kwa sasa, Mtibwa Sugar ipo nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 25 baada ya kushuka uwanjani mara 20 na kufanikiwa kuibuka na ushindi mara sita, sare saba na vipigo saba.
Maxime alisema haelewi ni kwa nini timu yake haipati matokeo mazuri licha ya kwamba imekuwa ikicheza soka safi pamoja na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga ambazo hata hivyo alidai hazitumiki.
CHANZO: MWANANCHI

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video