Saturday, March 8, 2014

Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
WAGONGA nyundo wa Mbeya, klabu ya Mbeya City wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya maafande wa Rhino Rangers katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara ndani ya dimba lao la Sokoine jijini Mbeya.
Mbeya City sasa imetimiza pointi 39, moja zaidi ya Yanga SC inayoshuka kwa nafasi moja hadi ya tatu, baada ya kucheza mechi 21. Yanga imecheza mechi 17.

Mabao ya Mbeya City leo yamefungwa na Saad Kipanga mawili dakika za nane na 24 na lingine Deus Kaseke dakika ya 34, wakati Yohana Maurice alijifunga dakika ya pili kuipatia Rhino bao la kuongoza.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, afisa habari wa Mbeya City, Fredy Jackson  amesema kuwa mchezo ulikuwa mgumu sana kwani Rhino waliingia uwanjani kwa lengo la kutafuta pointi tatu.
“Rhino wameonesha upinzani mkubwa sana katika mchezo wa leo. Walidhamiria sana kupata ushindi, lakini ubora wa wachezaji wetu umetusaidia”. Alisema Fredy.
IMG-20131029-WA0076Vijana wa kocha Juma Mwambusi wamewabamiza Rhino Rangers 3-1. Wasema safari yao bado inaendelea.
IMG_1615Coastal Union wakiwa katika dimba la nyumbani, CCM Mkwakwani jijini Tanga wameshindwa kutamba mbele ya wageni wao, Ashanti United wanaonolewa na kocha Abdallah King Kibaden `Mputa`.
Afisa habari huyo aliongeza kuwa mashabiki wa klabu hiyo walikuwa na hamu ya kuona timu yao inapata ushindi ikizingatiwa katika michezo miwili ya nyuma hawajapata pointi tatu.

“Dhamira ya Mbeya City iko pale pale, hatujakata tamaa ya ubingwa. Tunajiandaa kwa mechi zote na tuna matarajio ya kushinda mechi zote zilizosalia”. Aliongeza Fredy.

Naye kocha wa Rhino Rangers, Jumanne Chale alisema mchezo huo umekwenda salama na wamekubali matokeo ya mwisho.

“Tulipata nafasi za kufunga, lakini wachezaji wangu hawakuwa makini. Tumefunga bao moja na kufungwa matatu, sisi tunasonga mbele. Hakuna jinsi, sasa tunajiandaa kwa mchezo ujao”. Alisema Chale.

Huko Tanga wagosi wa kaya nao waliwakaribisha wauza mitumba wa Ilala, Ashanti United na kushuhudia mechi hiyo ikimalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Afisa habari wa Ashanti, Marijan Rajab ameufahamisha mtandao huu kuwa mchezo huo ulikuwa wa kawaida, na walipoteza nafasi za kufunga.

“Haikuwa mechi ngumu , tumepata nafasi kadhaa, kama wachezaji wangekuwa makini tungewalaza Wagosi wa Kaya nyumbani kwao”. Alisema Marijan.

Kwa upande wake, Hafidh Kido, afisa habari wa Coastal alisikitishwa na suluhu hiyo nyumbani kwani walijiandaa vizuri kushinda.

“Maandalizi yetu huwa ni mazuri siku zote, lakini imekuwa bahati mbaya kwetu. Tulikuwa na uwezo wa kuwafunga Ashanti kwa asilimia kubwa, lakini mpira una matokeo yake. Kikubwa tunaganga ya mbele”. Alisema Kido.

Dimba la mabatini lilihimili daluga za Ruvu Shooting dhidi ya JKT Oljoro na kushuhudia wenyeji wakishinda kwa bao 1-0.

Bao pekee la Ruvu Shooting lilifungwa dakika ya 63 na Ayub Kitala.

Afisa habari wa Shooting, Masau Bwire alisema waliingia uwanjani kwa lengo la kuzoa pointi tatu kufuatia kufungwa mechi mbili za nyuma.

“Hakika tulikuwa na hamu ya kupata ushindi. Oljoro walikuja kwa kasi kubwa wakihitaji pointi tatu, lakini uimara wa kikosi chetu na hamu ya kutafuta ushindi baada ya vipigo mfululizo umetusaidia sana”. Alisema Masau.

Masau alijigamba kuwa kikosi chao kimeonesha soka safi, japokuwa kimefunga bao moja.

“Wanaoifahamu Shooting, hakika inatandaza soka safi kabisa. Huko nyuma tulifumaniwa jamani. Sasa tumerejea katika msitari na ndio maana tumewanyoa kwa bao la Kitala”. Alisema Masau.

Kesho ligi hiyo itaendelea kwa mechi mbili kupigwa katika miji ya Dar es salaam na Mbeya.

Tanzania Prisons watakuwa nyumbani kukabilian na wekundu wa msimbazi Simba katika uwanja wa Sokoine.

Maafande wa JKT Ruvu watakuwa nyumbani, Azam complex jijini, kuwakabili Mtibwa Sugar.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video