Ndugu naomba kutumia nafasi hii
kutoa taarifa kuwa Mbeya City Fc hatukufurahishwa na aina ya mchezo wa kibabe
ulioonyeshwa na wachezaji wa club ya Rhino Rangers katika mechi iliyochezwa
jana jumamosi 8/3/2014 katika uwanja wa kumbukumbu ya sokoine Mbeya.
Nasema hivyo
kutokana na mchezo mbaya uliosababisha wachezaji wetu Richard Peter na Mwigane
Yeya kuumizwa vibaya kwa makusudi.
Richard aliumizwa vibaya na mlinda
mlango wa Rihno baada ya kumrukia kwa miguu yote miwili hivyo kusababisha madhara makubwa katika mbavu zake za kushoto.
Mchezaji huyu yuko kambini anaendelea na
tiba chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari kutoka hospitali ya rufaa Mbeya
pamoja na daktari wetu wa timu.
Na kwa upande wake Mwagane yeya aliumizwa
vibaya na huyo huyo mlinda mlango wa Rihno baada ya kumrukia vibaya na kumkwaruza
vidole macho yote mawili hivyo kumfanya mchezaji wetu kushindwa kuona kabisa na
anaendelea na matibabu chini ya doctor wetu.
Pamoja na hayo hatukufurahishwa kabisa na
nidhamu iliyoonyeshwa na mwalimu msaidizi wa club hiyo ambaye katika mchezo
mzima alikuwa akitamka maneno yasiyo na staha tofauti na mchezo wa mpira wa
miguu unavyoelekeza, na kwa kudhihirisha hilo baada ya mwalimu huyo kutolewa
kwenye benchi na mwamuzi alisikika akiwahamasisha wachezaji wake kuwaumiza
wachezaji wetu kwa kusema “wagongeni tu hao” na ndicho kilichotokea
Kwa maana hiyo basi kwa niaba ya club
tumeumizwa sana na aina isiyofaa ya uchezaji waliounesha wachezaji wa Rhino
Rangers na pia tunasikitika sana kuona aina hii ya uchezaji unaendelea
kufumbiwa macho. sisi Mbeya City Fc tunaamini nidhamu ndio ushindi.
Pamoja na yote tunaomba mamlaka zote
zinazohusika na VPL zikiongozwa na TFF waitazame upya mechi hiyo ili kulinda
nidhamu ya ligi kuu na kutoa maamuzi sahihi.
Ndugu mwana habari naomba pia kuweka sawa
mkanganyiko uliojitokeza jana kuhusu mfungaji wa goli la kwanza goli hilo
lilifungwa na Paul Nonga na si saady kipanga kama ambavyo vyombo vingi vya
habari vililiripoti.
ASANTENI
FREDDY JACKSON
Afisa habari MCC FC
0 comments:
Post a Comment