Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
WAGONGA nyundo wa Mbeya, klabu ya
Mbeya City wanaendelea kujinoa makali yao kuelekea mchezo ujao machi 16 dhidi
ya Maafande wa Jeshi la kujenga Taifa,
JKT Ruvu katika dimba la Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Afisa habari wa klabu hiyo, Freddy
Jackson amesema wachezaji wapo wapo katika hali nzuri na uimara mkubwa wa
kufanya vizuri mechi ijayo.
“Maandalizi yetu ni mazuri sana na tunaendelea kujiandaa
vyema ili kuhakikisha kuwa tunaibuka na pointi tatu muhimu katika mchezo huo
ambazo zitatuweka katika nafasi nzuri zaidi kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania
bara”. Alisema Freddy.
Afisa habari huyo aliwaomba mashabiki wao popote pale
walipo na watanzania kwa ujumla kuendelee kuwaamini kwani wanao uwezo mkubwa wa
kufanya vizuri zaidi.
Akizungumzia wachezaji wawili, Richard
Peter na Mwagane Yeya waliopata majeruhi katika mchezo uliopita, Freddy alisema
Peter hataweza kucheza mechi ijayo kwani
hali yake bado haijaimarika.
“Nikianzanza na
hali ya mchezaji Richard Peter aliyeumia katika mchezo kati yetu na Rhino
Rangers ya Tabora, mchezaji huyo hali yake bado haijatengemaa atakuwa nje kwa
wiki tatu zaidi chini ya uangalizi mkubwa wa daktari wetu hivyo basi atakosa
mechi ijayo . kwa ujumla mchezaji huyu bado ana
maumivu ya mbavu kutokana na kuumizwa vibaya katika mechi iliyopita”. Ilisema taarifa
ya Fredy.
Endeleeni kuwaamini vijana wenu |
Aidha Fredy aliongezaq kuwa mchezaji mwingine
Mwagane Yeya kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kuumizwa pia na mlinda mlango
wa Rihno siku hiyo hiyo.
“ Kutokana na hali yake inavyoendelea kuimarika mchezaji huyu
atatumika katika mechi ijayo na Ruvu JKT”. Alisema Freddy.
Mbeya City wapo
nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara wakiwa na pointi
39 nyuma ya Azam fc wenye pointi 40 kileleni.
Nafasi ya tatu
inashikiliwa na Yanga wenye pointi 38 lakini wamezidiwa michezo na klabu za
juu.
Nafasi ya nne wapo
Simba wenye pointi 36 kibindoni.
Wakati huo huo kocha
msaidizi wa Mbeya City FC Maka Mwalwisyi alisema sasa wameanza ligi upya baada
ya kufungwa na Yanga.
“Jinamizi la matokeo
dhidi ya Yanga liliwasumbua sana wachezaji wetu. Waliathirika sana kisaikolojia
na ndio maana wakafungwa tena na Coastal Union kule Tanga. Lakini sasa
tumejipanga upya na wimbi la ushindi lipo palepale”. Alisema Maka.
Aidha kocha huyo
aliwataka mashabiki kuwa na subira kwani Mbeya City FC ni klabu yenye malengo makubwa zaidi.
0 comments:
Post a Comment