Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
KIPIGO cha bao 1-0 walichopokea Simba sc kutoka kwa
Wagosi wa Kaya, Coastal Union ya Tanga
jana uwanja wa Taifa katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara kimezidi
kuwavuruga na kuwafanya wawe wanyonge ngwe hii ya lala salama.
Wagosi wa Kaya wakiwa katika morali ya ushindi ,
waliandika bao la ushindi dakika ya 45 kipindi cha kwanza kupitia kwa mlinzi
wake wa pembeni, Hamadi Juma kufuatia mabeki wa Simba kujikoroga.
Matokeo hayo yamepokewa kwa hisia tofauti na
mashabiki wa klabu hiyo ambao wanaona kama ligi kuu inawaonea msimu huu.
Hata hivyo Uongozi wa Simba sc kupitia kwa Afisa
habari wake, Asha Muhaji umewataka mashabiki na wanachama wao kuwa watulivu
katika kipindi hiki kigumu kwao.
“Matokeo ya jana hatukuyatarajia hata kidogo.
Tumeshitushwa mno na kipigo hicho. Lakini hayo ndio mambo ya uwanjani. Mpira
umechezwa vizuri na tumepoteza. Hatuna budi kuukubali ukweli japo unauma”.
Alisema Asha.
Mwamuzi vipi?: Kocha wa Simba sc, Dravko Logarusic (wa kwanza kulia) akiwa hailewi cha kufanya na kuonesha kuwa muda bado wakati mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho
Afisa habari huyo aliongeza kuwa kutokana na matokeo
wanayozidi kuyapata, yanawapa watu cha kusema, lakini soka huwa lina tabia ya
kupanda na kushuka.
“Siku za nyuma mashabiki wetu walikuwa wanatoka na
furaha uwanjani. Kwa sasa mambo yamebadilika. Huo ndio Mpira, ukiupenda lazima uwe
na moyo wa kukubaliana na kile kinachotokeo”.
Alisema Asha.
Asha alisisitiza kuwa bado wamebakiwa na mechi nne,
hivyo mashabiki waendelee kuiunga mkono klabu yao ili iweze kufanya vizuri.
“Mashabiki waliamini benchi la ufundi. Makocha
wataangalia wapi tumekosea ili kujipanga upya. Cha msingi tuwe wamoja katika
mechi zote”. Alisema Asha.
Baada ya kipigo cha jana, Simba wanaendelea kusalia
nafasi ya nne wakiwa na pointi zao 36, huku juu yake wakiwepo Mbeya City katika
nafasi ya tatu wajikusanyia pointi 42.
Mbeya City wameonekana kudhamiria kuwa miongoni mwa
timu tatu za juu, huku Mnyama Simba akihenyeka nyuma yao.
Wikiendi iliyopita walishinda mabao 2-0 dhidi ya JKT
Ruvu katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Dar es salaam.
Sady Kipanga ndiye alikuwa shujaa wa mechi hiyo na
kuwafanya mashabiki wa Mbeya City kuendelea kuwa na furaha msimu wao wa kwanza
katika michuano ya ligi kuu.
Ivo Vipo taulo baba?: Mwamuzi akimtaka kipa wa Simba sc, Ivo Mapunda kutoa taulo lake alilotundika langoni mwake
Simba Sc wanaonekana kupoteza matumaini kupata
nafasi tatu za juu.
Hata katika mchezo wa jana, baadhi ya dakika
wachezaji walionekana kutokuwa mchezoni, huku wakishindwa kutumia vyema nafasi
walizopata.
Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Croatia, Dravko Logarusic
anatakiwa kufanya kazi ya ziada kurudisha morali ya wachezaji wake wanaonekana
kukata tamaa.
Kipigo cha jana kimewavuruga zaidi Simba, lakini
Loga bado alisema wana matumaini ya kufanya vizuri katika mechi zilizosalia.
“Ligi ni ngumu msimu huu. Huwezi kuingia uwanjani
ukadhani utashinda kirahisi. Timu ndogo zimekuwa zikicheza vizuri na kuzipiga
timu kubwa. Kikubwa sisi tutakaa chini na kutafakari wapi kuna tatizo na
kulifanyia kazi”. Alisema Loga.
Simba baada ya mechi ya jana
amebakiwa na mechi tatu za ugenini na moja ya nyumbani.
Atakutana na Kagera Sugar ugenini mjini,
Bukoba. Pia atakuwa mgeni wa Azam na Yanga ingawa mechi zote zitachezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. harakati zao za kuwania ubingwa.
Mechi nyingine ni dhidi ya Ashanti
United katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Mechi dhidi ya Azam fc na Yanga
itakuwa ngumu zaidi kwa Simba kwasababu timu hizi zinahitaji matokeo kwa nguvu
zote katika
Pia Kagera Sugar wanapocheza Kaitaba
si rahisi kuwafunga, hivyo Loga lazima aandae majeshi yake vizuri.
Mechi na Ashanti United haitakuwa nyepesi
pia kwasababu wauza mitumba hao wa Ilala wapo katika harakati za kukwepa
kushuka daraja.
Benchi la ufundi la Simba lazima
litulize akili kwasababu mechi zilizosalia kwao ni ngumu.
0 comments:
Post a Comment