Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
0712461976 au 0764302956
BEKI wa FC Barcelona , Javier Mascherano amekiri kuwa mshambuliaji hatari wa Manchester City, Sergio Kun Aguero atakuwa hatari zaidi katika mchezo wa marudiano hapo a kesho ligi ya mabingwa barani ulaya (UEFA Champions League) katika dimba la Nou Camp ambapo Man City watahitaji kufuta kipigo cha mabao 2-0 walichopata katika mchezo wa kwanza nyumbani kwao, Etihad jijini Manchester.
City tayari wameshafika mchana wa leo nchini Hispania wakiwa na mlima mrefu wa kupanda kufuatia kupoteza mchezo wa kwanza nyumbani wiki tatu zilizopita.
Lakini mchezaji wa huyo wa zamani wa Liverpool, Mascherano aliwaambia waandishi wa habari katika mazoezi ya Barcelona wakati wa chakula cha mchana kuwa Aguero anaweza kubadili hali ya mambo katika mchezo wa marudiano hapo kesho endapo atapewa nafasi.
Mkweli: Javier Mascherano amekiri kumhofia Sergio Aguero
Maandalizi ya mwisho: Lionel Messi na wachezaji wenzake wakiwa mazoezini kujiandaa dhidi ya Manchester City
Neymar anatarajia kuonesha makali yake dhidi ya Manchester City katika dimba la Nou Camp kesho usiku
Mascherano alisema: “namjua Aguero vizuri na kwa maoni yangu ni moja kati ya washambuliaji bora watano duniani”.
“Ni mchezaji mkubwa na amepewa uwezo mkubwa, hivyo anaweza kuwa hatari sana kucheza naye”.
“Tutajitahidi kumkaba sana na kutokumpa nafasi kadri itakavyowezekana. Tutajaribu kutomuacha acheze kwa kujiachia”.
0 comments:
Post a Comment