Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
0712461976 au 0764302956
ZIKIWA zimesalia saa chache kushuhudia mechi ya marudiano baina ya Bayern Munich na Arsenal ligi ya mabingwa barani Ulaya usiku wa leo, mshambuliaji wa Munich, Mario Gotze amefurahia kukabiliana na rafiki yake wa zamani, Mesut Ozil, lakini ameonya kuwa leo Bayern hawatakuwa na huruma kama msimu uliopita.
Wakiwa na faida ya ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uwanja wa Emirates jijini London, vijana wa Pep Guardiola ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kufuzu hatua ya nane bora ya UEFA Champions League.
Washika bunduki wa London, Asernal wapo majaribuni leo hii dhidi ya mabingwa watetezi na Gotze amesisitiza kuwa hawatafanya makosa, hivyo haitakuwa rahisi kwa Aserne Wenger kushinda Allianz Arena.
Mario Gotze, anayeonekana na kiatu kipya cha Nike Magista amesema Bayern Munich usiku wa leo hawatakuwa na huruma hata kidogo kwa Asernal
Gotze anafurahia mafanikio mengine chini ya kocha wake Guardiola
Ndogo sana: Mchambuzi wa mechi wa Bloomberg Sports amewapa Arsenal asilimia 2.2 kuwatoa Bayern Munich usiku wa leo
“Mchezo wa marudiano dhidi ya Asernal utakuwa mgumu sana”. alisema Gotze katika mahojiano maalumu na Sportsmail.
“Lakini tutakuwa nyumbani, mashabiki wakiwa nyuma yetu, kwahiyo tunajiamini kuwa tutafuzu hatua ya robo fainali. Tunahitaji kushinda kila mchezo tunaocheza, hayo ndio malengo yetu”. Alisema Gotze.
Rejea nyuma: Katika mchezo wa marudiano mwaka jana, Olivier Giroud aliifungia Asernal mabao mawili katika dimba la Allianz Arena baada ya dakika tatu tu
Mzee wa balaaa: Mjerumani mwenzi na Gotze, Mesut Ozil alitazama jinsi penati yake ilivyookolewa katika uwanja wa Emirates (chini pichani)
0 comments:
Post a Comment