FURAHA
imerudi katika nafsi ya kocha David Moyes kufuatia Manchester United
kuifunga mabao 4-1 Aston Villa Uwanja wa Old Trafford jioni hii katika
mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Mabao
mawili yaliyofungwa na Wayne Rooney dakika za 20 na 45 kwa penalti na
mengine ya Juan Mata dakika ya 57 na Javier Hernandez dakika ya 90
yalitosha kuiongezea pointi United.
Villa ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Ashley Westwood dakika ya 13 kwa mpira wa adhabu.
United
sasa inatimiza pointi54 baada ya kucheza mechi 32 na inaendelea kubaki
nafasi ya saba nyuma ya Tottenham Hotspur yenye pointi 56 za mechi 31.
Babu kubwa: Wayne Rooney amefunga mabao mawili leo Manchester United ikiifunga Aston Villa 4-1

Juan Mata akipambana na Bacuna

Rooney akifunga kwa penalti
0 comments:
Post a Comment