Tuesday, March 25, 2014

MWENYEKITMwenyekiti wa Bunge Maalumla Katiba Samweli Sitta(wa pili kulia) akibadilishana na wajumbe leo mjini Dodoma mara baada ya kuharishwa kwa shughuli za Bunge hilo. Wengine ni Mjumbe   wa  Bunge hilo ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda(kulia),Captain Mstaafu John Komba , Erasto Zambi na Diana Chilolo.
Picha na Tiganya Vincent-Dodoma
……………………………………………………….
N a Magreth Kinabo ,Dodoma
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Samwel Sitta leo, ametangaza majina ya wenyeviti na makamu wenyeviti wa Kamati za bunge hilo.
 
 Majina hayo yametangazwa na Mwenyekiti huyo  baada ya uchaguzi wa viiongozi hao uliofanyika  (jana) Machi 24 , mwaka  2014 mjini  Dodoma .
 
Mwenyekiti ametangaza majina haya baada ya kuunda kamati hizo  jana kwa mujibu wa kanuni ya 54 (1) ya kanuni za Bunge Maalum za Mwaka 2014 ambazo zimetungwa chini ya kifungu cha 26 (1) cha sheria ya Mabadiliko ya Katiba sura ya 83, ambazo zinataja kuundwa kwa kamati 12 za Bunge Maalum.  
 
Wenyeviti na makamu wenyeviti waliochaguliwa katika kamati hizo ni pamoja na  Kamati  ya Uandishi ambayo Mwenyekiti   amechaguliwa Mhe. Andrew Chenge, Makamu wake ni Mgeni Hassan Juma. Kamati ya Kanuni Mwenyekiti ni Pandu Ameri Kificho, Makamu wake ni Dkt. Susan Kolimba. Kamati Na. 1 Mwenyekiti ni  Ummy Ally Mwalimu, na Makamu wake ni  Prof. Makame  Mbalawa
 
Wengine waliochaguliwa  katika Kamati Na. 2  ni  Shamsi Vuai Nahodha ambapo Makamu wake ni  Shamsa Mwangunga, Kamati Na. 3 Mwenyekiti ni  Dkt. Francis Michael, Makamu wake ni Fatma Mussa Juma.
 
Mhe. Sitta alisema waliochaguliwa katika Kamati Na. 4 Mwenyekiti ni  Christopher  Ole-Sendeka, Makamu wake ni  Dkt. Sira Ubwa Mamboya, Kamati Na. 5 Mwenyekiti ni  Hamad Rashid Mohamed Makamu wake ni  Assumpter  Mshama.
 
Waliochaguliwa katika Kamati Na. 6 Mwenyekiti ni Stephen Wassira na Makamu wake ni  Dkt. Maua Daftari, Kamati Na. 7  Mwenyekiti  Brig. Hassan Ngwilizi  ,Makamu wake  Waride BakariJabu, Kamati Na. 8 Mwenyekiti   ni Job Ndugai,Makamu wake ni Biubwa Yahya Othman.
 
Hali kadharika Kamati Na. 9 Mwenyekiti ni Kidawa Hamidi Saleh, Makamu wake Wiliam  Ngeleja, Kamati Na. 10 Mwenyekiti ni Anna  Abdallah, Makamu wake ni Salmin Awadh Salmin, Kamati Na. 11 Mwenyekiti ni  Anne  Malecela, Makamu wake  Hamad  Masauni na Kamati Na. 12 Mwenyekiti  niwake  Paul  Kimiti na Makamu wake ni  Thuwaybah E. Kisasi.
 
Aidha, kwa uchaguzi huo, Mhe. Sitta  alitangaza wajumbe wa Kamati ya  Uongozi ya Bunge Maalum la Katiba ambao  ni wenyekiti wote wa kamati hizo wakiwemo wajumbe wengine watano aliowateua kwa mujibu wa Kanuni.
 
Wajumbe hao walioteuliwa na Sitta kuingia katika kamati hiyo ni pamoja na Fakharia Khamisi Shomari, Mary Chatanda, Profesa Ibrahim Lipumba, Amon Mpanju na Hamoud Abuu Juma. Hata hivyo pamoja na majina hayo kutangazwa Profesa Lipumba alisimama na kujitoa katika nafasi hiyo hivyo kufanya nafasi za uteuzi kuwa nne badala ya Tano .

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video