Kikosi cha Mtibwa Sugar
Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
KATIKA hali isiyo ya kawaida, Mabingwa wa Tanzania
kwa mwaka 1999 na 2000, Mtibwa Sugar ya
Manungu Turiani mkoani Morogoro wamekata tamaa ya kushika nafasi tano za juu
katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu.
Tobias Kifaru Lugalambwike, msemaji wa Mtibwa
amesema kuwa kwasasa wanapigania nafasi ya sita au saba kwasababu hawana uwezo
wa kupanda nafasi za juu.
“Mashabiki wetu watambue kuwa ligi imekuwa ngumu
zaidi msimu huu. Mtibwa hatuna chetu kwasasa zaidi ya kung`ang`ania nafasi ya
sita au saba. Nafasi ya kwanza, pili, tatu, nne, tano ni ngumu kwetu”. Alisema
Kifaru.
Kifaru alisema mpaka sasa wameshuka dimbani mara 22 na kujikusanyia pointi 27 katika nafasi ya 8,
na kwa michezo waliyosaliwa nayo wanatarajia upinzani mkubwa kupata matokeo.
“Tumerejea nyumbani kuendelea na mazoezi kujiandaa
dhidi ya Coastal Union. Wapinzani wetu wametoka kushinda dhidi ya Simba sc,
sisi tulitoka sare ya 1-1 na Mgambo kule Tanga. Mipango yetu ni kupambana hapa
kwetu kuchukua pointi tatu muhimu”. Alisema Kifaru.
Mtibwa Sugar wamebakiza mechi ya machi 30 dhidi ya
Coastal Union katika dimba la Manungu, pia watasafiri mpaka mkoani Tabora
kuwavaa vibonde, Rhino Rangers aprili 6 mwaka huu.
Baada ya Tabora, watarudi Manungu aprili 12 kuwakaribisha
maafande wa Ruvu Shooting.
Watahitimisha msimu aprili 19 mkoani Arusha ambapo
watawafuata maafande wa JKT Oljoro.
Mmewazodoa bao 1-0 Simba sc Taifa jumapili, vipi Mtibwa sugar machi 30 Manungu?
Nao Coastal Union kupitia kwa Afisa habari wake,
Hafidh Kido wametangaza kiama kwenye mechi nne zilizosalia.
Akizungumza kwa kujiamini, Kido alisema kikosi chao
kimechanganyika kwa wakongwe na damu changa, hivyo kukifanya kuwa na kasi kubwa.
“Uliona jinsi timu ilivyocheza dhidi ya Simba,
hakika kumekuwepo na mabadiliko. Tunajiandaa dhidi ya Mtibwa Sugar kule
Manungu, lazima tuibuke na ushindi”. Alisema Kido.
Afisa habari huyo alisema kuwa wamebakiza mechi
dhidi ya Mtibwa Sugar machi 30 mwaka huu katika uwanja wa Manungu Turiani
mkoani Morogoro.
Pia watakuwa na mchezo wa aprili 6 mwaka huu dhidi
ya ndugu zao Mgambo JKT katika uwanja wa CCM Mkwakwani, jijini Tanga.
Baada ya mechi hiyo Wagosi hao wa Kaya
watawakaribisha tena JKT Ruvu katika dimba lao la Mkwakwani.
Mechi ya mwisho itakuwa aprili 19 mwaka huu ambapo
wataumana na Kagera Sugar katika dimba la Mkwakwani, Tanga.
0 comments:
Post a Comment