Diwani wa Kata ya Kabungu Kasonso akiwasilisha hoja katika vikao vyao vya maamuzi kuhusu Halmashauri kuhamia Kabungu.
(PICHA NA KIBADA WA KIBADA MPANDA KATAVI)
……………………………………………………….
Na Kibada Kibada -Katavi
Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Mpanda limesema kuwa haliwezi kutengua maamuzi yake ya awali ya baraza iliyoyapitisha katika kikao kilichopita ya kuamua ujenzi wa makao mapya ya Halmashauri hiyo kuwa Kata ya Kabungu Tarafa ya Kabungu mahali ilipoanzia Wilaya ya Mpanda tangu kuanzishwa kwake mwaka 1947 enzi za ukoloni.
Hayo yamebainishwa kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika jana kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri,.
Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa na madiwani hao, wameeleza kuwa maamuzi yaliyopitishwa na wajumbe wa kikao hicho katika vikao vyao vya nyuma hayawezi kubadilishwa kwa kuwa yalikuwa maamuzi halali ,sahihi na ya kisheria.
Awali Diwani wa Kata ya Kabungu Selemani Kasonso aliyetaka kupata ufafanuzi kutoka kwa mwenyekiti kama maamuzi yaliyopitishwa ya kujengwa kwa halamshauri yao Kata ya kabungu yametenguliwa, au bado yako vilevile au yako kama yalivyoamuliwa , kwa kuwa tangu kuweka mauzi hayo miezi sita haijafika.
Akaongeza kuwa kutenguliwa kwake hadi miezi sita ifike hivyo hayawezi kutenguliwa, na kama watatengua watakuwa wamekiuka kanuni, taratibu na kuvunja sheria.
Akizungumzia maamuzi hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda Yasini Kibiriti alieleza kuwa suala la kujenga makao makuu ya Halmashauri yatabaki palepale Kata ya Kabungu kama ilivyoamuriwa katika vikao vilivyopita.
Kibiriti aliendelea kusema kuwa suala hilo lilianza kujadiliwa kwa kuwashirikisha wananchi kuanzia ngazi zote kupitia vikao halali vya kamati ya maendeleo ya kata, pia kwa kuwashirikisha viongozi na wataalam ili kupata maamuzi ya wananchi kwa kuzingatia taratibu zote.
Alieleza kuwa iliundwa kamati ya watalaam waliozungukia kila kata na Tarafa kupata Maoni ya wananchi ambapo wananchi walipendekeza Makao Makuu yajengwe Kata ya Kabungu na si sehemu nyingine kwa kuzingatia vigezo na vipaumbele na mambo muhimu kwa maslahai walivyoona na Histori ya Wilaya hiyo.
Kwa mjibu wa Kanuni na sheria za vikao vinavyoongoza Halmashauri, maamuzi yanapopitishwa na baraza la madiwani hutenguliwa hadi ipite miezi sita , sasa tangu kupitishwa kwa maamuzi hayo ya kuamua kujengwa makao makuu Kabungu bado miezi sita haijafika, iweje kutengua mamuzi hayo na kufanya hivyo ni kuvunja sheria.
Kwa kauli moja madiwani walikubaliana kuwa maamuzi yao yatabaki kama yalivyoamuriwa na ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Mpanda yatajengwa kabungu na si mahali pengine.
0 comments:
Post a Comment