FT: DAKIKA 90 SIMBA SC 0 VS 1 COASTAL UNION
Dakika ya mwisho kabisa, Ramadhan Singano amekosa bao la wazi.
Dakika za lala kwa buriani Simba wanakosa bao
Dakika za lala salama, (dk 45) Simba sc wanakosa mipango
Dakika ya 40 Simba sc 0 vs 1 Coastal Union
Dakika ya 38 Mkude anaachia shuti kali, linatoka nje ya lango
Taifa: Dakika ya 37 Coastal Union wanapata kona, lakini haizai matunda baada ya kipa Ivo Mapunda kuudaka mpira
..........................
Kutoka Mabatini, Ruvu Shooting 2 vs o Ashanti United
...............
Dakika ya 28 Simba wanashambulia kama nyuki, lakini Mosoti anakosa bao.
Dakika ya 26 Simba wanapata kona, Mkude amepiga shuti limegonga mwamba
Dakika ya 23 Simba wanafanya shambulizi zuri, lakini kipa wa coastal anaokoa na kuwa kona, hata hivyo haizai matunda
Dakika ya 22 kipindi cha pili bado Simba wapo nyuma kwa bao 1-0
Dakika ya 17 Haruna Shamte anakwedna benchi anaingia Edward Christopher
Dakika 17 Coastal wanapata kona, lakini haizai matunda.
Dakika ya 16, Simba sc bado wapo hoi uwanja wa Taifa
Dakika ya 13 Simba hawajaona lango na Coastal wanaongoza kwa bao 1-0
Dakika ya 11 kipindi cha pili, Amisi Tambwe anakosa bao la wazi kufuatia krosi ya Wilium Lucian `Galas`
Mpira umesimama uwanja wa Taifa
Mpira umeanza na sasa ni dakika ya kwanza kipindi cha pili
Omary Salum anatoka kwa upande Simba anaingia Wilium Lusian `Galas`.
Timu zote ndio zinaingia uwanjani muda huu uwanja wa Taifa Kuanza kipindi cha pili
.................................................
Kutoka Mabatini mkoani Pwani, Mpira ni mapumziko, Ashanti United wapo nyuma kwa bao 1-0 kutoka kwa wenyeji Ruvu Shooting.
..............................................
Kwa ujumla katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, Timu zote zimecheza mpira mzuri, lakini beki ya Simba Sc haijatulia kwasababu inajichanganya mara kwa mara.
DAKIKA 45 ZA KIPINDI CHA KWANZA ZIMEMALIZIKA, SIMBA SC 0 VS 1 COASTAL UNION
Dakika ya 45 Coastal Union wanafunga bao la kuongoza kupitia kwa Hamadi Juma kwa baada ya mabeki wa Simba SC kujichanganya
Dakika ya 24, Haruna Chanongo anakosa bao la wazi
Dakika ya 23, Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Henry Joseph anaingia Said Ndemla.
Dakika ya 6 kipindi cha kwanza hakuna bao kwa timu zote
Sekunde ya 1, Mpira umeanza hapa uwanja wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment