…………………………………………….
Na Kibada Kibada -katavi
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sasi Salula amefanya ziara ya kutembelea miradi inayofadhiliwa na ofisi yake katika ukanda wa Ziwa Tanganyika Wilayani Mpanda Mkoani Katavi na kujionea hali halisi ya miradi inavyoendelea kutekelezwa na kagiza kukamilika mapema iwezekanavyo.
Agizo hilo amelitoa baada ya kukuta baadhi ya miradi ikiwa katika hali isiyoridhisha na kupata hofu kama inaweza kukamilika kwa wakati ili kwenda sawasawa na mkataba na wafadhili, hivyo akaagiza zichukuliwe hatua za haraka kukamilisha miradi hiyo kabla ya muda kuisha.
Miradi hiyo inasimamiwa na program ya uendelezaji na Uhifadhi mazingira wa Bonde la ziwa Tanganyika katika mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi , na makao makuu ya miradi hiyo iko mkoani kigoma na ofisi ya makamu wa Rais ndiyo inayosimamia .
Amesema watu wanaoishi Nchi zinazozungukwa na ziwa Tanganyika wanakaribia karibu milioni kumi, na wanakabiliwa na changamoto ya uharibifu wa mazingira, hivyo hatua za makusudi zisipochukuliwa kuhakikisha mazingira ya ziwa hilo yanahifadhiwa huenda uchumi wa wananchi hao hasa wale wanaotegemea ziwa Tanganyika ukawa mashakani.
Aliitaja miradi ya inayotekelezwa kwa upande wa mkoa wa Katavi Katika wilaya ya Mpanda , ukanda wa Ziwa Tanganyika kuwa ni miradi ya Elimu , Afya, Maji na Ujenzi wa Mwalo unaojengwa kwenye kijiji cha Ikola Kata ya Ikola kwa thamani ya shilingi milioni 800, fedha zilizotolewa na wafadhili kwa ajili ya kuwaletea Maendeleo wananchi wanaozunguka ukanda huo.
Akiwa katika Kijiji cha Ikola kukagua ujenzi wa Mwalo ameitaka Halmashauri kusisimamia ujenzi wa mwalo huo na kukamilika mara moja kabla ya muda uliopangwa na wafadhili kumalizika.
Mkandarasi anayejenga mwalo ameshalipwa kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya kazi iliyofanyika hadi hapo ilipofikia ikiwa ni pamoja na ujenzi wa soko la kuuuzia samaki, na maeneo mengine muhimu.
0 comments:
Post a Comment