Bondia
Japhet Kaseba ameahidiwa gari endapo atamzimisha bondia Thomas Mashali
katika pambano lao la machi 29, ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es
salaam. Bondia huyo amesema maandalizi yake yanakwenda barabara.
Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
HOMA
ya pambano la masumbwi baina ya Japhet Kaseba dhidi ya Thomas Mashali
litakalofanyika machi 29 katika ukumbi wa PTA sabasaba jijini Dar es
salaam kuwania ubingwa wa UBO Afrika Kilo 79 inazidi kupanda , huku
maandalizi yakienda vizuri kwa mabondia hao pamoja na mabondia wengine
watakaopigana siku hiyo kutoka mkoani Tanga.
Katibu
mkuu wa shirikisho la ngumi Tanzania PST, Antony Luta ameuambia mtandao
huu kuwa hamasa imekuwa kubwa kwa mabondia baada ya wadau wa mchezo
huo kuwaahidi zawadi baadhi yao endapo watapata ushindi.
“Siku
mbili tatu hivi, tumepata hasama sana baada ya msanii wa zamani wa
maigizo, Doti Nata Poshi ambaye amejitokeza na kumuahidi Kaseba gari
endapo atampiga. Zawadi hii amemuahidi Kaseba tu, kama atapigwa basi
ataondoka na gari yake. Hii ni hamasa kubwa sana”. Alisema Luta.
Thomas Mashali atakuwa na kibaru kizoto cha kumuonesha umwamba Japhet Kaseba
Luta
alisema kaseba kuahidiwa gari itakuwa chachu kubwa kwake kutafuta
ushindi kwa nguvu zote, hivyo pambana litakuwa kali sana na mashabiki
wajitokeze kwa wingi siku hiyo.
Katibu huyo aliongeza kuwa nao mabondia wa Tanga
wameahidiwa pikipiki maarufu kwa jina la Bodaboda kama wataibuka na ushindi
katika mapambano yao.
“Kiukweli wanapojitokeza watu kama hawa
kutoa zawadi kwa mabondia, sisi watu wa masumbwi tunajisikia furaha sana. Kwa
siku nyingi sana tumeachwa kama yatima”. Alisema Luta.
Luta aliwataja mabondia wa Tanga kuwa ni
Alan kamoti atakayepambana na Fadhil Ally wa Dar es salaam ubingwa wa UBO
raundi 10.
Mwingine kutoka Tanga waja leo waondoka
leo ni J.J Ngotoka atakayepanda ulingo dhidi ya Fredy Sayuni wa Dar es salaam ubingwa wa UBO
raundi 8.
Wengine ni Aji Juma atakayeoneshana kazi
na Juma Fundi pambano la raundi 8.
Naye Shaban Dunga atapanda ulingoni
kutunishana msuli na Joki Hamis.
Luta aliwaomba wadau na wadhamini wa
michezo kujitokeza katika mchezo wa masumbwi kwani ni mchezo unaoweza kuliletea
sifa taifa la Tanzania.
“Mchezo wa masumbwi ni mchezo wa siku
nyingi, lakini wadhamini wametutupa mbali sana na inaonekana kama hauna maana.
Cha msingi tunawaomba waje kwa wingi ili tuweze kufanikisha malengo yetu”.
Alisema Luta.
Wakati hayo yakiendelea, bondia Japhet
Kaseba amesema maandalizi yake yanakwenda vizuri huku akiwaahidi mashabiki wake
ushindi.
“Binafsi namheshimu sana Mashali, lakini
kutokana na maandalizi yangu nitafanya vizuri na namuomba mungu anisaidie”.
Alisema Kaseba.
Simu ya Mashali haijapatikana mpaka
tunaingia mtamboni, lakini tutamtafuta kujua anaendeleaje na mazoezi.
0 comments:
Post a Comment