RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ameendelea kuongoza kura za kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka linalotarajia kuanza Aprili 20 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Kikwete anaongoza kwa kura zaidi ya milioni 6.9 ambazo hazijafikiwa na wengine wanaopigiwa kura kuwa wageni rasmi katika tamasha hilo.
Msama alisema wengine wanaomfuatia Kikwete kuwania nafasi hiyo ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa huku Mwenyekiti wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
Wengine wanaopigiwa kura ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe, Mkurugenzi wa Kampuni za IPP, Dk Reginald Mengi na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Aidha Msama alitoa wito kwa mashabiki kuendelea kupiga kura kuchagua mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo ni kwa ajili ya kumuimbia na kumtukuza Mungu kupitia waimbaji mbalimbali wa Kitaifa na Kimataifa.
0 comments:
Post a Comment