Mashabiki wa Manchester United wanaochukizwa
na mwenendo wa timu yao chini ya uongozi wa David Moyes wamefanikiwa
kupata ndege itakayopita juu ya paa la uwanja wa Old Trafford jumamosi
hii - huku ndege hiyo ikiwa imebeba bango la ‘Moyes Out’.
Ndege
hiyo imepangwa kupita juu ya paa la OT kwa dakika 10 kabla ya mchezo
kuanza na baadae kwa dakika 5 na wakati wa mchezo dhidi ya Aston Villa.
Kundi la mashabiki hao tayari limethibitisha kwamba kesho ndege hiyo yenye bango la “Wrong One: Moyes Out.”
Bango hilo ni kinyume ya lile walilotaka kulishusha kutoka kwenye jukwaa la Stretford End linalosomeka ‘Chosen One’.
0 comments:
Post a Comment