Thursday, March 27, 2014

???????????????????????????????Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya akiwaongoza madiwani kuelekea wodini kuwasalimia wagonjwa waliolazwa kwa lengo la kuwapa  pole na misaada mbalimbali kisha kujionea hali halisi ya huduma wodini hapo
(Picha zote na Kibada wa Kibada Mpanda Katavi)
……………………………………………….
Na Kibada Kibada –Katavi.
Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi inayohudumiwa na Halmashauri  ya Wilaya ya Mpanda  inakabiliwa na changamoto lukuki za upungufu wa dawa, watumishi ,vifaa vya kufanyia kazi, na huduma nyingine muhimu hali inayochangia utoaji wa huduma  kuwa mgumu.
Hayo yamebainishwa na Madiwani wa Halmashauri hiyo waliofanya ziara ya kutembelea Hospitali hiyo kujionea changamoto zinazoikabili hospitali na kujionea hali halisi inayoikabili ili kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizi.
Akitoa taarifa ya hali ya Hospitali hiyo Kaimu  Mganga Mkuu wa Halmashauri  Joseph Msemwa alieleza kuwa kwa wastani hali ni ngumu kwa Hospitali ya wilaya kwa kuwa inakabiliwa na chanagamoto za aina mbalimbali katika utoaji wa huduma kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi.
Dkt Msemwa alieleza kuwa  upungufu wa watumishi  unachangiwa na mgawanyo ulifanyika kwa kugawa Halmashauri mbili za Mlele na Nsimbo ambapo watumishi wengi wamehamishwa na hakuna mbadala hivyo waliobakia kuw wachache.
 Changamoto nyingine iliyopo ni upungufu wa wodi za kulaza wagonjwa , vitanda, mashuka vyandarua na vifaa vingine vya kutolea huduma ya tiba. 
Alieleza kuwa pamoja na Halmashauri kujitahidi kutoa huduma za  fedha za uendeshaji lakini bado mzigo unaielemea Halmashauri ya Mpanda Pekee inazidiwa kutokana na wingi wa wagonjwa wanaokuja kupata huduma.
  Akashauri kuwa ni vyema Halmashauri zote zikaona uwezekano wa kuchangia fedha za uendeshaji kwa vile wagonjwa wengi wanaohudumiwa katika hospitali hiyo wanatoka Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Awadh   aliyewaongoza madiwani hao katika ziara hiyo alisema wamejione hali halisi na wao kama wawakilishi watalifanyia kazi suala hilo kwa lengo la  kulipatia ufumbuzi
Naye Muuguzi wa Hospitali hiyo, Devota Mhagama akizunguza katika wodi ya akina mama na watoto alieleza kuwa  hali inatisha kutokana na   uwezo  mdogo wa wodi ambayo ina uwezo wa kulaza   wagonjwa 39 kwa kuwa kuna vitanda 39 tu, lakini wakati mwingine wanalaza hadi watoto 60  mara mbili zaidi ya uwezo wake.  

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video