Lori la kubeba taka likiwa eneo kituo cha gereji barabara ya mandela ,huku likiwa limebeba uchafu baada ya kuharibika na limekaa hapo siku mbili.
Huo unaonekana kwa juu ni uchafu uliooza na unatoa harufu kali kituoni hapo. eneo la kituo cha gereji mandela road
Uchafu uliobebwa na Lori hilo,lililoharibika eneo la kituo cha gereji mandela road

Mwandishi wa blog hii nilishuhudia mwenyewe na kupiga picha pia kuonja adha ya harufu kali inayotoka kwenye gari hiyo.Manispaa ya kinondoni na wasimamizi wa usafi mnaombwa kufuatilia hili na kuweza kulitatua kwani ni kero kwa watumiaji wa kituo hiki.
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA DJ SEK BLOG
0 comments:
Post a Comment