BALAA!. mechi ya 1,000 kwa Kocha wa Asernal akiiongoza klabu hiyo, Mfaransa Aserne Wenger imemalizika kwa kupewa gharika ya mabao 6-0 na Mreno Jose Mourinho katika mechi ya ligi kuu soka nchini England leo hii uwanja wa Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Siku moja baada ya Wenger kukabidhiwa tuzo ya dhahabu kwa kuiongoza Arsenal katika mechi 1,000 tangu aanze kazi, leo alitoka Uwanja wa Stamford Bridge akiwa kichwa chini na asiye na hamu kwa kipigo kikali kutoka kwa chelsea.
Mwezi uliopita, aliitwa mtaalamu wa kushindwa na kocha Jose Mouringi kwani amejaribu kushinda taji kwa mara 11 mfululizo bila mafanikio.
Mfaransa huyo alionekana hana matumaini baada ya dakika 15 za kipindi ch kwanza kujikuta akiwa nyuma kwa mabao mawili ya Samuel Eto’o na Andre Schurrle.
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia baada ya kuwaliza Asernal mabao 4-0 kipindi cha kwanza
Gharika: Wachezaji wa Chelsea wakisahangilia bao la 6 lililofungwa na Mohamed Salah
Mcameroon Samuel Eto’o alitangulia kuifungia The Blues dakika ya tano kwa pasi ya Andre Schurrle, ambaye yeye mwenyewe akafunga la pili dakika ya saba kwa pasi ya Nemanja Matic kabla ya Edin Hazard kufunga kwa penalti dakika ya 17.
Penalti hiyo ilifuatia Alex Oxlade-Chamberlain kuushika mpira kwa makusudi akiokoa shuti la Edin Hazard, lakini ajabu refa akampa kadi nyekundu Kieran Gibbs.
Zikiwa zimesalia dakika tatu kabla ya mapumziko, Oscar aliifungia Chelsea bao la tatu kwa pasi ya Fernando Torres, ambaye naye alipokea krosi ya Andre Schurrle.
Kipindi cha pili, Chelsea walirudi na moto ule ule na dakika ya 66 Oscar aliifungia The Blues bao la tano kwa shuti la kawaida akiwa ndani ya eneo la hatari, ambalo lilionekana kama kipa Szczesny angeweza kuokoa, lakini akatunguliwa, kabla ya Mohamed Salah kufunga la sita dakika ya 71.
Kwa matokeo hayo, Chelsea inazidi kujiwekea zege kileleni kwa kutimiza pointi 69 baada ya mechi 31 na Arsenal inabaki na pointi zake 62 baada ya mechi 30.
Bao la mapema: Samuel Eto’o akishangilia bao la dakika ya tano katika ushindi wa mabao 6-0 kwenye uwanja wa Stamford Bridge
Nyundo ya pili: Schurrle akifumua shuti lililozama na kuifanya Chelsea iwe mbele kwa mabao 2-0
0 comments:
Post a Comment