>>JUMAPILI MACHI 23 SAA 5 USIKU, SANTIAGO BERNABEU, MADRID
VIGOGO wa Spain, Real Madrid na Barcelona, wanakutana leo Usiku kwenye Mechi ya La Liga ambayo Wachambuzi wanadai ndio itatoa mwelekeo nani Bingwa Msimu huu.
Real wako kileleni mwa La Liga wakiwa Pointi 3 mbele ya Atletico Madrid na Barca wapo Nafasi ya 4, Pointi 1 nyuma ya Atletico.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
LA LIGA
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
F
|
A
|
GD
|
PTS
|
1
|
Real Madrid CF
|
28
|
22
|
4
|
2
|
77
|
26
|
51
|
70
|
2
|
Atletico de Madrid
|
28
|
21
|
4
|
3
|
64
|
21
|
43
|
67
|
3
|
FC Barcelona
|
28
|
21
|
3
|
4
|
81
|
22
|
59
|
66
|
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Makocha wa Timu hizi, Tata Martino wa Barca na Carlo Ancelotti wa Real, watakuwa kwenye El Clasico yao ya Pili huku Mastaa wao, Gareth Bale wa Real, akitegemea kuicheza kwa mara ya Kwanza na Neymar wa Barca kutinga kwa mara ya Pili.
Wakati Real Madrid wanamtegemea sana Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, ambae ndie Mfungaji Bora kwenye La Liga akiwa na Bao 25 [Ana Jumla ya Bao 41 Msimu huu], Barca wanae Lionel Messi ambae kwenye La Liga yupo Nambari 3 katika Ufungaji [Wa Pili ni Diego Costa mwenye Bao 23] akiwa na Bao 18 licha ya kukosa Mechi 9 akiwa Majeruhi 25 [Ana Jumla ya Bao 26 Msimu huu].
Timu hizi zitakutana tena kwenye Fainali ya Copa del Rey hko Valencia hapo Aprili 16.
Hali za Wachezaji
REAL MADRID
Fowadi wa Real, Karim Benzema, hakucheza Mechi ya Jumanne siku ya UEFA CHAMPIONZ LIGI walipoifunga Schalke akiwa ni Majeruhu na huenda akaikosa Mechi hii.
Nae Jese Rodriguez hataweza kucheza baada kuumia Goti walipocheza na Schalke na
Na anaungana na Majeruhi mwingine Alvaro Arbeloa kuwa nje.
BARCELONA
Barcelona itamkosa Nahodha wao Carles Puyol ambae ni Majeruhi na tayari ameshatangaza kustaafu mwishoni mwa Msimu huu.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Real Madrid [Mfumo: 4-2-3-1]: Lopez,
Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo;
Xabi Alonso, Luka Modric,
Isco; Gareth Bale, Cristiano Ronaldo,
Morata
Barcelona Madrid [Mfumo: 4-3-3]:
Valdes,
Jordi Alba, Pique, Bartra, Mascherano,
Xavi , Iniesta, Busquets,
Messi , Neymar , Sanchez,
LA LIGA
Uso kwa Uso
26/10/13, 18:00 FC Barcelona 2 - 1 Real Madrid
02/03/13, 16:00 Real Madrid 2-1 FC Barcelona
07/10/12, 19:50 FC Barcelona 2-2 Real Madrid
21/04/12, 20:00 FC Barcelona 1-2 Real Madrid
10/12/11, 22:00 Real Madrid 1-3 FC Barcelona
16/04/11, 22:00 Real Madrid 1-1 FC Barcelona
29/11/10, 21:00 FC Barcelona 5-0 Real Madrid
10/04/10, 22:00 Real Madrid 0-2 FC Barcelona
29/11/09, 19:00 FC Barcelona 1-0 Real Madrid
02/05/09, 20:00 Real Madrid 2-6 FC Barcelona
13/12/08, 22:00 FC Barcelona 2-0 Real Madrid
07/05/08, 22:00 Real Madrid 4-1 FC Barcelona
23/12/07, 19:00 FC Barcelona 0-1 Real Madrid
10/03/07, 22:00 FC Barcelona 3-3 Real Madrid
22/10/06, 21:00 Real Madrid 2-0 FC Barcelona
01/04/06, 22:00 FC Barcelona 1-1 Real Madrid
19/11/05, 20:00 Real Madrid 0-3 FC Barcelona
10/04/05, 19:00 Real Madrid 4-2 FC Barcelona
20/11/04, 22:00 FC Barcelona 3-0 Real Madrid
25/04/04, 19:30 Real Madrid 1-2 FC Barcelona
0 comments:
Post a Comment