MCHEZAJI bora wa dunia, Cristiano Dos Santos Aveiro Ronaldo ameifungia mabao mawili timu yake ya Taifa ya Ureno ikifumua mabao 5-1 Cameroon katika mchezo wa kirafiki uliopigwa jana usiku na kufanikiwa kuwa mchezaji aliyeifungia mabao mengi zaidi Ureno kihistoria.
Ronaldo sasa amefikisha jumla ya 49 aliyoifungia Ureno, mawili zaidi ya Pauleta aliyekuwa anaongoza.
“Sina wasiwasi wa kuvunja rekodi, ni vitu ambavyo vinakuja vyenyewe, kwa baraka tele”, alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akihojiwa na Televisheni ya RTP.
Cameroon ilimaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza ikiwa imefungana bao 1-1 na Ureno, lakini kipindi cha pili ikabugizwa nne ndani ya dakika 18.
Ronaldo alianza kufunga dakika ya 21, Aboubakar akaisawazishia Cameroon dakika ya 43 na kipindi cha pili Meireles akaifungia Ureno dakika ya 66, akifuatiwa na Coentrao dakika ya 67, Edinho dakika ya 77 na Cristiano tena dakika ya 83.
Ronaldo akipambana na Allan Nyom kwenye chaki jana
0 comments:
Post a Comment