CHELSEA imetanua mbawa zake kileleni mwa Ligi Kuu ya England, kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tottenham Hotspur Uwanja wa Stamford Bridge usku wa jana.
Mabao ya The Blues leo yamefungwa na Samuel Eto'o dakika ya 56, Edin Hazard dakika ya 60 na Demba Ba mawili dakika za 88 na 89.
Ushindi huo, unaifanya Chelsea itimize pointi 69 baada ya kucheza mechi 28 na kujiimarisha kileleni, ikiizidi kwa pointi saba Liverpool iliyo nafasi ya pili kwa pointi zake 59 sawa na Asrenal, nao wakiwa wamecheza mechi 28 pia. Manchester City ni ya nne sasa kwa pointi zake 57, lakini ina mechi mbili mkononi.
Mimi kizee; Eto'o akishangilia kama mzee baada ya kufunga kuwabeza wanaomuita mzee kwenye timu hiyo, baada ya kocha Jose Mourinho pia kusema ana umri mkubwa |
Eto'o akitumia mwili wake kumtoka Michael Dawson
Samuel Eto'o akimzunguka kipa Lloris
Eto'o alianguka mara kadhaa jana
0 comments:
Post a Comment