Wednesday, March 12, 2014

Mkurugenzi wa Oparesheni wa chama cha demokrasia na maendeleo katika uchaguzi wa Kalenga Benson Kigaila aliyesimama kwa nyuma akizungumza na mratibu wa kampeni ccm Kalenga Miraj Mtaturu  kulia kwake ni mratibu wa uchaguzi wa ccm Taifa Edwin Millinga.
……………………………………………………….
Na Bashir Nkoromo, Iringa
WAWAKILISHI wa Chadema wakiongozwa na Mratibu wa Kampeni za chama hicho katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Benson Kigaiya leo wameumbuka baada ya kushindwa kuonyesha mbele ya jombo la Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) sheria ambayo wawakilishi hao wa Chadema waling’ang’ania kuwa ipo kuwaruhusu wafuasi wa vyama kukaa mita mia kusubiri matokeo au kulinda kura.

Chadema walizidi kutahayari kiasi cha mwanasheria wa chama hicho, John Malya, aliyeambatana wa wawakilishi hao, kwenye mkutano wa Tume na vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo utaofanyika Machi 16, mwaka huu, naye kukiri kwamba hakuna sheria ambayo awali ilikuwa imedaiwa na Kigaia kuwa ipo.
“Madai haya ya kuwepo sheria inayoruhusu wafuasi au kundi la watu kukaa mita mia kutoka kituo cha kupigia kura kwa lengo lolote ikiwepo kusubiri matokeo au kulinda kura, yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na baadhi ya vyama vya siasa, lakini nasi tumekuwa tukiwaambia kwamba hakuna sheria hiyo, na kuwataka yeyote anayejua kifungu cha sheria hiyo atuonyeshe, Kigaia wewe unasema ipo hebu tuonyeshe kifungu hicho”,  alisema, Mjumbe wa Tume hiyo Jaji Mstaafu John Mkwawa.

Mapema Kigaia alisisitiza kuwa kwa upande wa Chadema wanaona kuwa sheria ipo na kutokana na kuwepo sheria hiyo, kwa hiyo itakuwa ni haki ya msingi kwa wafuasi wa chama hicho kukaa mita 100, wakisubiri matokeo ya kura zao na pia kulinda ukiukwaji wowote unaoweza kufanyika kwa watu kutoa rushwa au kupiga kampeni za chini chini wakati wa uchaguzi.

Maelezo hayo ya Kigaia yalipingwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, akisema, sheria iliyopo ni inayotaka kuanzia mita mia moja kutoka kituo cha kupigia kura pasiwepo nembo au ishara zozote za utambulisho wa chama chochote kinachoshiriki uchaguzi.

Akitoa taarifa ya Tume hiyo kwa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo ambavyo ni CCM, Chadema na CHAUSTA, Mwenyekiti wa Tume, pamoja na mambo mengine, alisema, mi marufuku kwa kundi au mtu yeyote kukaa kwenye kituo cha kupigua kura au karibu na kituo hicho baada ya kupiga kura.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video