Kutoka soka in bongo
MASHINDANO makubwa ya Klabu Barani Afrika, CAF CHAMPIONZ LIGI na Kombe la Shirikisho, Wikiendi hii walicheza Mechi zao za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Mabingwa Watetezi wa CAF CHAMPIONZ LIGI, Al Ahly ya Misri, ambao Raundi iliyopita waliwatoa Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, kwa Mikwaju ya Penati baada kwenda Sare ya Jumla ya Bao 1-1 katika Mechi mbili, walianza Ugenini huko Libya na kuchapwa Bao 1-0 na Al Ahli – Benghazi.
Nao TP Mazembe ya Congo DR, Klabu yenye Mastraika wawili Mashujaa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta, ilicheza Ugenini huko Ivory Coast kwa kucheza na Sewe Sport na kufungwa Bao 2-1.
Mechi nyingine ya mvuto ilikuwa ni ile kati ya Nkana FC ya Zambia na Magwiji wa Egypt, Al Zamalek iiliyochezwa huko Zambia na kutoka 0-0.
Nayo Klabu nyingine ya Congo DR, AS Vita, ikicheza Nyumbani iliwanyuka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini Bao 3-0.
CAF CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
Ijumaa Machi 21
Al Ahli - Benghazi – Libya 1 Al Ahly – Egypt 0
Nkana FC – Zambia 0 Al Zamalek – Egypt 0
AS Bamako – Mali 1 Espérance Sportive de Tunis – Tunisia 1
Jumapili Machi 23
AS Vita Club - Congo, DR 3 Kaizer Chiefs - South Africa 0
AC Leopards de Dolisie – Congo 1 Al-Hilal – Sudan 1
Sewe Sport - Ivory Coast 2 TP Mazembe - Congo, DR 1
Horoya Athlétique Club – Guinea 0 Club Sportif Sfaxien – Tunisia 1
Entente Sportive de Sétif - Algeria 1 Coton Sport FC – Cameroon 0
Marudiano
Machi 29
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Al Ahly – Egypt v Al Ahli - Benghazi – Libya [0-1]
Al Zamalek – Egypt v Nkana FC – Zambia [0-0]
Coton Sport FC – Cameroon v Entente Sportive de Sétif – Algeria [0-1]
Espérance Sportive de Tunis – Tunisia v AS Real de Bamako – Mali [1-1]
Club Sportif Sfaxien – Tunisia v Horoya Athlétique Club – Guinea [1-0]
Al-Hilal – Sudan v AC Leopards de Dolisie – Congo [1-1]
TP Mazembe - Congo, DR v Sewe Sport - Ivory Coast [1-2]
Kaizer Chiefs - South Africa v AS Vita Club - Congo, DR [0-3]
++++++++++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU:
-DROO YA KUPANGA MAKUNDI Tarehe 29 Aprili 2014
-MAKUNDI YATAKUWA MAWILI YA TIMU 4 KILA MOJA NA KUCHEZA MTINDO WA LIGI, NYUMBANI NA UGENINI
-WASHINDI WAWILI WA JUU WA KILA KUNDI WATAINGIA NUSU FAINALI
++++++++++++++++++++++++++++++++
CAF KOMBE LA SHIRIKISHO
Raundi ya Mtoano ya Timu 15
Jumamosi Machi 22
Al Ismaily – Egypt 0 Petro Atlético de Luanda – Angola 0
E.S. Sahel – Tunisia 1 Supersport United - South Africa 0
Warri Wolves – Nigeria 0 C. A. Bizertin – Tunisia 0
Wady Degla – Egypt 2 Djoliba AC - Mali 0
AS Kigali – Rwanda 1 Difaa Hassani El Jadidi – Morocco 0
Medeama – Ghana 2 ZESCO United FC – Zambia 0
How Mine – Zimbabwe 2 Bayelsa United – Nigeria 1
Jumapili Machi 23
CS Constantine – Algeria 1 ASEC Mimosas Abidjan - Ivory Coast 0
Marudiano
Machi 30
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Djoliba AC – Mali v Wady Degla – Egypt [0-2]
Petro Atlético de Luanda – Angola v Al Ismaily – Egypt [0-0]
Supersport United - South Africa v E.S. Sahel – Tunisia [0-1]
Difaa Hassani El Jadidi – Morocco v AS Kigali – Rwanda [0-1]
ZESCO United FC – Zambia v Medeama – Ghana [0-2]
C. A. Bizertin – Tunisia v Warri Wolves – Nigeria [0-0]
ASEC Mimosas Abidjan - Ivory Coast v CS Constantine – Algeria [0-1]
**Ratiba inaweza kuwa na Mabadiliko
0 comments:
Post a Comment