Wednesday, March 12, 2014

1 (4)Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fisoo akizungumza na wadau wa filamu nchini (hawapo pichani) wakati akipitia na kukagua filamu ya Dark Forest ya Kikundi cha Harakati kwenye ofisi za Bodi hiyo jijini Dar es Salaam leo.
2 (2)Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fisoo akiwaeleza jambo Mkurugenzi wa Kikundi cha Harakati Fatia Musa (katikati) na Mjumbe wa kikundi hicho na Mwigizaji wa filamu hiyo Ramadhani Nassoro kuhusu filamu yao inayoitwa Dark Forest, kwenye ofisi ya Bodi hiyo jijini Dar es Salaam leo.7 (1)Mkurugenzi wa Kikundi cha Harakati Fatia Musa, akitia saini makubaliano ya kutekeleza maazimio waliokubaliana na Bodi kuhusu kurekebisha filamu hiyo huku akishuhudiwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini Joyce Fisoo.
8Mwigizaji wa filamu hiyo Ramadhani Nassoro, akitia saini makubaliano ya kutekeleza maazimio waliokubaliana na Bodi kuhusu kurekebisha filamu hiyo huku akishuhudiwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini.
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO.
……………………………………………………………………………………………….
Hussein Makame-MAELEZO
BODI ya Filamu imewaonya wazalishaji wa filamu nchini kuwa watakaotengeneza filamu chini ya kiwango kwa makusudi watafungiwa ikiwa ni moja ya njia ya kuboresha tasnia ya filamu nchini na kukuza vipaji vya wasanii wachanga.
Onyo hilo limetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fissoo baada ya kupitia na kuikagua filamu ya Dark Forest ya Kikundi cha Harakati ambayo imeonekana imetengenezwa chini ya viwango vinavyotakiwa.
Alisema utengenezaji wa filamu hiyo haikutumia vifaa vya kitaalamu, ina mwanga mbaya, haikutumia vifaa vya sauti vya kitaalamu na kufanya kuingiliana kwa sauti nyingine zisizohitajika na kasoro nyingine nyingi.
Fissoo alisema Bodi hiyo pia ilibaini  kuwa uchukuaji wa picha wa filamu hiyo ulitumia siku tatu jambo ambalo ni kuidhalilisha tasnia ya filamu na kutowatendea haki Watanzania ambao ndio watumiaji wa kazi hiyo.
“Baada ya kupitiwa ilibainika filamu hiyo kuwa katika kiwango cha chini sana na kwamba Kampuni ya Lee One Production ilishiriki kuchukua picha zake ni kampuni yenye uzoefu na kazi zake zilikwishawahi kuja Bodi zikiwa katika kiwango cha kuridhisha” alisema Fissoo.
Akizungumza kwa njia ya simu na MAELEZO, Mkurugenzi wa Lee One Production Emmanuel Mapunda alisema awali filamu hiyo ilirekodiwa vizuri lakini kanda ya picha za filamu hiyo haikutunzwa kwenye vifaa bora kama alivyoshauri.
Alisema baada ya kugundua kuwa picha za filamu hiyo zimeharibika, aliwashauri wahusika wa filamu hiyo kutoitoa kutokana na kutokuwa na viwango vinavyohitajika na kwamba wanatakiwa wakairekodi upya, hata hiyo hawakukubaliana.
Kutokana na filamu hiyo kutengenezwa chini ya kiwango, Fissoo aliitisha kikao kukutana na kikundi cha Harakati kilichotoa filamu hiyo na wahusika wote kujadiliana nao kwa kina, walifikia maazimio kuwa tabia ya kuharibu kwa makusudi kazi za wasanii wanaoibukia iachwe mara moja.
“Wanaotengeneza filamu chini ya kiwango kwa makusudi watafungiwa, onyo kali kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Lee One Production na Mwongozaji wa filamu husika Bwana Ramadhani Kishoka kwa kutotekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi na taalum” alisema Fissoo na kuongeza :
”Marekebisho hayo yafanyike kwa kuzingatia viwango vya ubora kwani kuipeleka sokoni filamu hiyo ni kutowatendea haki Watanzania na kuiua tasnia ya filamu jambo ambalo Serikali haitaliruhusu”.
Waandaaji wa filamu hiyo walikiri kuwa kiwango cha filamu hiyo ni cha chini na muongozaji wake Ramadhani Kisoka ameahidi kuwa ataandika barua ya kuomba radhi na kurudia kazi hiyo na kuiwasilisha Bodi.
Bodi ya Filamu imekuwa ikitekeleza majukumu yake ikiwemo kupitia na kukagua filamu zinazotengenezwa nchini na kuzipitisha kwenda sokoni ambapo filamu hiyo ya Dark Forest ilikamatwa na Bodi wakati wa operesheni zake za kawaida.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video