Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
KIKOSI cha wachezaji
wa vinara wa ligi kuu soka Tanzania
bara, Azam fc kimeondoka leo asubuhi
Jijini Dar es Salaam kwa basi lake
kwenda Tanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji MgamboJKT,
utakaochezwa kesho Jumatano kwenye
Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya Azam fc, wachezaji ambao wataukosa mchezo huo ambao ni majeruhi
na hawajaambatana na timu Tanga ni, SamihHaji Nuhu, Joseph Lubasha Kimwaga,
Ibrahim Mwaipopo, Farid Mussa na Ismail Gambo.
Azam fc mpaka sasa
wamejikusanyia pointi 47 kileleni baada ya kushuka dimbani mara 21.
Nafasi ya pili wapo
Yanga wenye pointi 43 baada ya kushuka dimbani mara 20, lakini kesho timu zote
zinakabiliwa na mechi.
Yanga watakuwa na
kibarua kizito uwanja wa Taifa dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons,
wajelajela.
Azam fc wataingia
katika mchezo wa kesho wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya JKT
Oljoro katika uwanja wao wa Azam Complex.
Mabingwa watetezi
Yanga wenyewe walikuwa mjini Tabora ambapo walishinda mabao 3-0 dhidi ya
waburuza mkia katika msimamo, Rhino Rangers.
Afisa
habari wa Azam fc, Jafar Idd Maganga aliuambia mtandao huu kuwa kwasasa kila
mechi kwao ni fainali.
“Hatuna cha kuhitaji zaidi ya kuandika historia mpya
katika soka la Tanzania. Mpaka sasa hatujafungwa katika michezo 21. Tunatafuta
pointi tatu kwa Mgambo hapo kesho ili kujiweka katika mazingira mazuri ya
kutwaa Taji kwa mara ya kwanza msimu huu”. Alisema Jafar.
Jafar aliongeza kuwa wachezaji wao wanaelewa wazi
majukumu yao na ndoto za klabu msimu huu,
hivyo imekuwa rahisi kwa kocha mkuu, Mcameroon, Joseph Marius Omog kuwaweka
mchezoni muda wote.
“Mashabiki wetu waendelee kutuunga mkono mpaka
mwisho. Dhamira yetu ipo wazi. Tunatambua ugumu wa mechi ya kesho kwasababu
Mgambo wanakwepa kushuka daraja. Tutajitahidi kuwa bora zaidi yao ili kuibuka
na ushindi”. Alisema Jafar.
Naye kocha msaidizi wa Mgambo JKT, Moka Shaban
Dihimba aliueleza mtandao huu kuwa wamejipanga vilivyo katika mechi hizi za
mwisho ili kubakia ligi kuu.
“Mzunguko wa kwanza tulikuw a katika hali mbaya
sana. Lakini ngwe hii ya pili tumejidhatiti na kufikisha pointi 19 katika
nafasi ya 11. Malengo yetu ni kufanya vizuri mechi zilizosalia kuanzia ya kesho
dhidi ya Azam fc”. Alisema Moka.
Kocha huyo alikiri ugumu wa mechi hiyo kwasababu
Azam fc ni timu nzuri ambayo haijapoteza mechi yoyote mpaka sasa.
0 comments:
Post a Comment